Muundo Na Mtindo Wa TECNO-Camon CM
Ni wazi kwamba TECNO wamekua wakifanya vyema katika
uzalishaji na uuzaji wa simu janja zenye
sifa za kipekee na ubora wa hali ya juu, Camon CM ndo toleo jipya kutoka
TECNO kwa mwaka 2018 . Ufuatao ni uchambuzi wa mtindo na muundo wa TECNO-Camon
CM
MUONEKANO
Kwa mara ya kwanza nilivyoiona Camon CM niliifananisha na
iphone 7 namna umbo lake ilivyo, ni nyembamba milimeta 5.6 [visual slim] inajaa
kiganjani hivyo ni fahari na rahisi kuibeba mkononi
KIOO
Camon CM ina ukubwa wa skrini inchi 5.7 chenye uwiano wa
18:9, nikatazama filamu na kusoma kurasa mbalimbali kwa wigo mpana zaidi pasipo
mipaka ya kuta za simu
BETRI
Baada ya kutazama filamu na kusoma kurasa mbali mbali,
nilisikiliza miziki kwamuda mrefu usiopungua masaa 2 lakini bado nilibakiwa na
kiasi kikubwa cha chaji 40%
No comments