Breaking News

Naibu Meya Ilala Kumbilamoto Kukabidhi Mashine Ya Pamu.

Naibu meya wa Halmashauri ya Manspaa ya ilala Omary Kumbilamoto anataraji kukabidhi msaada wa mashine ya kutibu pumu katika zahanati ya vingunguti.  

Akizungumza jijini dar es salaam, Mhe kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya vingunguti alisema mashine hiyo alinunua nchini dubai, baada ya kuona umuhimu wa uhitaji katika zahanati yake.

“Wananchi wangu, hasa wenye pumu ilikuwa inawalazimu kuchoma sindano, lakini mashine hii itasaidia kutoa matibabu bila mgonjwa kuchomwa sindano” alisema Meya Kumbilamoto.

Alisema amepanga kukabidhi mashine hiyo kwa uongozi wa zahanati hiyo ndani ya wiki hii.
Aidha Naibu meya kumbilamoto aliongeza kuwa mashine hiyo ya kisasa yeye binafsi anaamini itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari za pumu kwa wananchi wake na kuhaidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo katika zahanati hiyo kwa kadri ya uwezo wake ili wananchi wake wapate huduma bora za afya zinazo stahili.

Katika jitihada za kuhakikisha anaboresha huduma mbalimbali kwa wananchi wa kata ya vingunguti  hususani afya Naibu meya Omary Kumbillamoto tayali ameshakabidhi gari ya kubebea wagonjwa ambalo ni tegemeo katika halmashauri ya Manispaa Ya Ilala.

No comments