CUF Lipumba Washtukia Rafu Uchaguzi Kinondoni.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni CUF Lipumba, Rajab Juma akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu mapema leo 18 Jan 2018 jijini dar
es salaam.
******
Chama cha Wananchi (CUF)
upande unaomuunga mkono Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba umemteua RAJAB JUMA aliyekuwa
kampeni meneja wa aliekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho Maulid
Mtulia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni.
Akizungumza
mapema leo jijini dar es salaam mara baada ya kuchukua Fomu ya kugombea ubunge
kupitia chama hicho mgombea huyo ametoa angalizo kufatia kuonekana kuwepo na
viashiria vya kutokkuwa huru kufatia kitendo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
Bw Mtulia kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM) tayali ameshaanza kampeni.
“Mtulia
ameanza kupita katika matawi ya CUF kuomba kuungwa mkono na wanachama wa chama katika matawi mbali mbali ya chama hicho katika manspaa ya kinondoni hatua
ambayo ni sawa na kuanza kampeni mapema kabla ya wakati uliopangwa na tume ya
uchaguzi. Alisema Bw Juma.
Mgombea Ubunge
Jimbo la Kindondoni CUF Rajab Juma akikabidhiwa fomu na msimamizi
msaidizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni Latifa Ramadhani mapema leo 18 Jan 2018 jijini Dar es salaam.
*******
Alisema ameamua kulizungumzia swala hilo mapema hivyo kama hatua za makusudi azitachukuliwa litaleta
athari kwani siasa siyo chuki, uadui amedhamiria kufanya siasa kama sehemu
ya kuweza kuondo na kutatua kero zinawakabili wananchi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa habari na Uenezi wa CUF Lipumba, Bw. Abdul Kambaya alisema
kitendo cha CCM kumteua Mtulia ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
“kitendo kilichofanywa na Mtulia cha kujizulu uanachama na kupoteza nafasi ya ubunge, ukizingatia haumwi, hana tatizo la kutohudhuria bungeni na kupelekea kurudiwa kwa uchaguzi mdogo usiokuwa na sababu, ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kutumika kutatua kero za wananchi kama kununua madawa, ujenzi wa miundombinu pamoja na maji” alisema Kambaya.
Aidha Bw. Kambaya aliongeza kuwa chama kiejipanga kuhakikisha
wanashinda katika uchaguzi huo kutokana na kuwa na mgombea mzuri, mwenye uwezo,
anaekubalika na wananchi na mwenye kujiamini.
Uchaguzi
mdogo wa marudio katika jimbo la kinondoni unatarajiwa kufanyika Februari 17,
2018 mwaka huu.
No comments