Hatma Ya Waliofukuzwa Kwa Vyeti Feki, Na Vyeti Vya Darasa La 7
HATIMA ya
mafao ya wafanyakazi wa serikali walioondolewa kwenye ajira kutokana na
kubainika kuwa na vyeti feki itajulikana kabla ya Bunge la Bajeti, imefahamika.
Hatua
hiyo inatokana na serikali kujibu hoja nane za Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (Tucta) na kwamba suala la kulipwa au kutolipwa haki zao
litafahamika Machi au Aprili, mwaka huu.
Hoja
zingine ni ajira ya waliomaliza darasa la saba, kupandishwa madaraja, madeni ya
wafanyakazi, nyongeza za mishahara, kutofanyika vikao vya bodi, kujua idadi ya
taasisi zilizoundwa na kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Katibu
Mkuu wa Tucta, Dk. Yahya Msigwa, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mamlaka
mbalimbali zinamalizia kulifanyia kazi suala la vyeti feki na kwamba kabla ya Mei
Mosi, mwaka huu, hatima yao itakuwa imepatikana.
“Unajua
kilichofanyika ni kosa la jinai na la kinidhamu, hivyo sisi Tucta tunaendelea
kuiomba serikali angalau wapatiwe kifuta machozi,” alisema.
Alisema
ajira kwa waliomaliza darasa la saba Serikali ilitoa waraka unaosema watumishi
wa umma wanapaswa kumaliza elimu ya kidato cha nne kuanzia Mei, 20, 2004.
Pia
alisema baada ya hapo, walitakiwa kujiendeleza ili kuwa na vigezo vya kuendelea
kuwa watumishi wa umma iwapo zipo baadhi ya idara zinawahitaji na kujenga hoja.
Kuhusu
kupandishwa madaraja,
Dk.
Msigwa alisema watumishi wengi hawajapandishwa kutokana na uhakiki wa vyeti,
hivyo serikali imetenga fedha kwa ajili ya mpango huo kwa kutegemea bajeti
ijayo.
Alisema
malipo yataanza tangu siku ya kupata barua ili kupunguza madeni ambayo inadaiwa
na kwamba kimsingi katika hilo, yako madeni ya mishahara na isiyo ya mishahara.
Kuhusu
madeni, kwa mujibu wa Dk. Msigwa, serikali imesema imemaliza uhakiki na imeanza
kulipa lakini itakuwa vigumu kulipa watu wote kwa mkupuo bali watazingatia
uhakiki ya madeni yenyewe.
Kwa
upande wa nyongeza ya mishahara, alisema Rais John Magufuli hakuahidi wakati wa
sherehe za Mei Mosi bali nyongeza hiyo italolewa mwaka huu.
Aidha,
Dk. Msigwa alisema hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na
mifuko miwili, mmoja wa binafsi na mwingine wa umma, imetokana kauli za
wafanyakazi wenyewe kwenye sherere za Mei Mosi.
Alisema
rasimu iliyotegenezwa si mbaya licha upungufu uliopo na wanaendelea kutoa maoni
kabla muswada haujawasilishwa Bungeni.
No comments