Kutoka Mwanza: Afariki Kwa Kugongwa Na Ndege Ya FASTJET
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-bE5yFv9P7G-jlNPjQSabX03-a7xIbJShbAGGw2u7vTMRp-b18CQftMconYjPD667gF9JtbnAGl8OkxDYudNC8vUqZYZVBXomTM08O4EMuQMpCQ3RbJaZlsagCCQgEoPAQh9asMpBDev2/s640/1.jpg)
Mkazi
mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet
iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini Dar es Salaam.
Kaimu
MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard
Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.
Amesema
ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa
mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.
“Ingawa
ndege ndiyo ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au
kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege ndiyo
kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema Mayongela.
Amesema
kabla ya ndege hiyo kuruka, taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo
kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.
“Haijulikani
mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio
kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi
utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.
Amesema
kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi
kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama uwanjani hapo.
“Pengine
tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa ujenzi na
upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia katika njia ya
kurukia ndege,” amesema.
Ili
kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama
kwenye viwanja vya ndege nchini.
Chanzo- Mwananchi
No comments