Home
/
KITAIFA
/
Ivi Ndivyo Aliyepiga Picha Majengo Yenye Nyufa Udsm Anusurika Kutekwa Na Wasiojulikana
Ivi Ndivyo Aliyepiga Picha Majengo Yenye Nyufa Udsm Anusurika Kutekwa Na Wasiojulikana
4 hrs ·
Toka Mwaka jana mwezi wa 12 baada ya mimi kupiga picha katika
mojawapo ya Hostel za Dr. John Pombe Magufuli iliyokuwa ikionyesha nyufa
kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakinifuatilia mara kwa mara kila mahali
ninapoenda, (Siwezi kusema kupiga picha za nyufa ndio sababu ya kunifuatilia
kwangu au la), awali nilidhani labda wanashughuli zao lakini kilichonishangaza
ni kuwa kila siku zinavyoidi kwenda nikikaa sehemu watu hawa nao walikuwa
wanakaa umbali kidogo nilipo mimi, nami nikianza kuondoka nikigeuka nyumba
nabaini kuwa wananifuatilia.... Siku zinavyozidi kwenda nimebaini watu wale
walikuwa na nia mbaya kwangu.
Wiki jana, siku ya Alhamisi nikiwa natoka Mlimani City nilianza
kutembea kurudi zangu hosteli nikipita ile njia ya Service road mbele yangu
niliona gari aina ya Noah imepaki na mlango ukiwa wazi (Mbele kidogo ya geti la
Mlimani City) nilivyofika kwenye ile gari watu wale walinitaka niingie kwenye
gari huku wakiwa ndani ya gari lile! Mimi niliwajibu, "Mnanifahamu??....
Mnajua ninakoenda??...... Wakati nikiwauliza haya maswali walianza kushuka
kwenye gari huku wakiniambia sio lazima kutujua sisi ni akina nani...... "
Ingia kwenye gari haraka" waliniambia kwa ukali.
Namshukuru Mungu kulikuwa na watu jirani wakiwemo wakiwemo
waendesha bajaji waliokuwa wamepaki nyuma kidogo, hivyo nilipiga kelele
kuwaeleza kuwa wanataka kuniteka.
Baada ya mimi kupiga kelele watu wale waliokuwa wanashuka
kunitaka kunilazimisha niingie kwenye gari waliingia haraka na kuliondosha gari
lile.... Kipekee niwashukuru waendesha bajaji kwa msaada wenu, hakika
msingekuwepo nyinyi pale leo tungekuwa tunazungumza mengine.
Baada ya tukio lile niliripoti kwenye vyombo tofauti vya ulinzi
ikiwa ni pamoja na Polisi wasaidizi (Auxiliary Police) na Polisi wenyewe na
kuandikiwa RB yenye kumbukumbu namba UD /RB/344/2018...... Polisi waliniomba
endapo nitaziona sura zile mahali popote zikinifuatilia nitoe taarifa huku
wakiniomba nisitembee peke yangu kila sehemu ninapoenda na kunieleza kuwa
nitakapoona inafaa nijilinde.
Hali kadhalika suala hili niliripoti kwa walezi wangu wanaonilea
kwa maana ya Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi hapa chuoni kwangu.
Rai yangu kwa nyie vipele mnaonifuatilia waambieni hao wanao
watuma wauache utoto....... Mlimpa nini Kumbusho Dawson mpaka mnamfatilia
hivi??? kama mnanidai njooni nitawalipa.
Shame be upon you!!!!
Shubamitiiiiiiiiii.
Shubamitiiiiiiiiii.
Ivi Ndivyo Aliyepiga Picha Majengo Yenye Nyufa Udsm Anusurika Kutekwa Na Wasiojulikana
Reviewed by Harakati za jiji
on
January 19, 2018
Rating: 5
No comments