WAZIRI KAIRUKI: WATUMISHI HEWA NA VYETI FEKI BADO NI CHANGAMOTO
Waziri
nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala
bora Mhe. Angela Kairuki amesema Serikali bado inakabiliwa na
changamoto kubwa ya watumishi wenye kughushi vyeti pamoja na watumishi hewa
ambao walikuwa wakiendelea kupokea mshahara.
Akizungumza katika mkutano wa watumishi wa umma wa wilaya ya
Kinondoni kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili alisema wapo baadhi ya
watumishi waliokuwa wakilipwa mishahara ambao walishafariki na wengine tayali
ni wastaafu pamoja na wasio na vyeti halali.
Alisema
kwa kutambua hilo serikali ilianzisha zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumshi wa
umma kote nchini zoezi ambalo limekuwa likifanyika kwa umakini mkubwa kupitia
mfumo wa kanzidata kwa kushirikiana na RITA na TRA.
Aidha amewataka watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea
na badala yake wafanye kazi kwa mujibu wa sheria na kuzingatia maadili ya kazi
hili kuongeza ufanisi zaidi.
Waziri Kairuki ametoa onyo kwa watumishi wa
umma wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kuvujisha za taarifa ya serikali kuacha
mara moja vinginevyo wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
Katika hatua nyingine waziri Kairuki Ametoa wito kwa watumishi
wa umma kubadili mfumo wa maisha yao ili kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi na
mengineyo yanayoambukiza sambamba na kufanya mazoezi ili kukabiliana na
magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na presha.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amezitaja
changamoto zinazoikabili wilaya ya Kinondoni kuwa ni upungufu wa watumishi
katika idara ya Ardhi ambao wako nane tu hivyo amemuomba Waziri Kairuki
kushughulikia suala hilo ili kurahisisha utendaji kazi katika wilaya hiyo
sambamba na kusema kuwa jumla ya watumishi 144 wa sekta ya afya katika wilaya
yake wamekutwa na vyeti feki.
Ziara hii ni mwendelezo wa ziara za Waziri Kairuki mkoani Dar es
salaam kujadili changamotombalimbali zinazowakabili tayali amefanya ziara katika wilaya ya Temeke, Mbagala, Kigamboni na
sasa Kinondoni ili kuzungumza na watumishi wa umma
No comments