NEWS UPDATES: TRA LEO YAZIPIGA KUFULI OFISI ZA KAMPUNI YA SAHARA MEDIA GROUP INAYOMILIKI VITUO VYA STAR TV NA RADIO FREE AFRICA (RFA)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheE51Dbfc3srNM0a8yHhCXhWncM19c1q8PB0PR0OZ2zcPIxvMl4Kp351JIvF67K5NZ4IlVhSikAogEwQ1-DTkC8YQOHNuCuAaJOqy7OdA3J_Bg0M8Q3n8FpuLX8WfNYctQvDdsqOpwsPES/s640/1.jpg)
Ofisi za Kampuni ya Sahara Media
Group inayomiliki kituo cha televisheni cha Star na cha redio cha Radio Free
Africa (RFA) zimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa deni la Sh4.5
bilioni.
Ofisi hizo zimefungwa leo Alhamisi
(Julai 13) na wakala wa TRA, Kampuni ya Sukah Auction Mart and Court Brokers ya
jijini Mwanza.
Meneja utumishi na utawala wa Sahara
Media Group, Raphael Shilatu amesema ni kweli wana malimbikizo ya madeni
yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.
No comments