Breaking News

CUF YA LIPUMBA YALAANI HUJUMA ZINAZOFANYWA NA CHADEMA KUPITIA MGOGORO WAO WA UONGOZI.

Chama cha wananchi (CUF) kimelaani hujuma zinazofanywa kupitia matamko mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi  wa chama cha chama cha democrasia ba maendeleo (CHADEMA) kuingilia mambo ya chama kwa kutumia mgogoro uongozi uliopo ndani ya chama hicho.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Kaimu  Katibu Mkuu Cuf Taifa Bi. Magdalena Sakaya alisema viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa kushirikiana na Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad wamekuwa wakitumia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa lengo la kutaka kuifuta CUF upande wa Tanzania bara.
Alisema hujuma zinazopangwa ni pamoja na kuvamia ofisi ya makao makuu ya chama hicho buguruni na sasa wameenda mbali zaidi na kuamua kujitokeza kwenye kesi zilizofunguliwa na washirika wao dhidi ya viongozi wa CUF kuwa nhujuma hizo azitafanikiwa kamwe.
Bi  Sakaya amekitaka Chama hicho kujikita katika kutafuta sababu za wanachama na viongozi wao kuhama katika chama chao na kujiunga na chama cha CCM na si kuingilia kati mgogoro wa CUF ambao kimsingi hauwahusu.
Aidha aliongeza kuwa uwepo wa viongozi wa CHADEMA mahakamani katika kesi zilizofunguliwa chama hicho ni ushahidi tosha wa maazimio ya vikao vyao vya kutaka kukihujumu chama cha wananchi CUF na kuongeza kuwa chama hicho ndio wanahusika wakuu wa mgogoro unaoendelea ndani ya  CUF.
Mhe. Sakaya amewakata wanachama wa CUF kuendelea kuwa watulivu kwani chama hicho kipo katika mikono salama na kamwe njama zote zinazopangwa za kutaka kukihujumu chama hicho azitafanikiwa kwani wao wanatekeleza na kukilinda chama kwa mujibu wa katiba ya chama.

No comments