TCRA: MARUFUKU MATANGAZO KWENYE MIITO YA SIMU
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-b6MzgEwBaVMEO6mph3GV0ksjTdVUXCx3eQ8RDjQhy6skGyxVMvCYSr699wLTr9J020vMhTkc6JbapkUbC4N7e7-_PMV1riph37LcPb5iwIcmmQJki7mAyx_FDTZCLuQ2g9jeww6fBmQW/s640/1.jpg)
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), imepiga marufuku matangazo ya biashara yanayowekwa mtumiaji anapopiga
simu ili kutoa fursa kwa watumiaji kupata mawasiliano bila usumbufu.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James
Kilaba amesema jana (Ijumaa) kuwa mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi kutoka
kwa watumiaji wa simu wakilalamikia matangazo hayo yanayotolewa na kampuni za
simu.
Amesema tayari TCRA imeshaziandikia
barua kampuni zote za simu kusitisha matangazo hayo na itakutana nazo kwa
majadiliano ya kina Julai 6.
Amesema mamlaka haitambui utaratibu
huo na inauchukulia kama kero kwa watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia
njia hiyo ya mawasiliano kurahisisha mambo.
“Tuna imani mtu anapopiga simu ana
shida ya haraka na anahitaji afanye mawasiliano, unapomuwekea matangazo kwa
dakika tatu au nne ni usumbufu,” amesema.
Katika siku za karibuni imekuwa ni
kawaida kwa mtu anayepiga simu kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye
kuambiwa namba anayopiga haipatikani.
No comments