KAULI + VIDEO: ALICHOSEMA MHE NDUGAI MARA BAADA YA KUITWA DHAIFU,"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdbiS9Lk5xjttx6YBEPzsaPLvzWskFND4SPJqQ0hGJG4Qa0g-vvOkomBjQBlC33_26yru1J9H_sFPjfLaDFCwb4ayVVZ4TF-d2PceCw9K7xNJKTNzDew3RkcCgflqMbhIJrD31Q6Pf_8b6/s640/1.jpg)
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa wabunge wanaodai kuwa bunge ni
dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa kauli za
kudhihaki chombo hicho.
Mhe. Ndugai amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao pamoja na kwa serikali kwa ujumla.
"Yupo mwenzetu alisimama hapa na
kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni yangu hizi ni lugha za kuudhi
kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa na watu wakaletwa hapa halafu
wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi.
"Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa nafasi mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema Ndungai

Pamoja na hayo, Ndugai ameendelea kwa
kusema "Katika bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia
na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili
ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye
ulazima tutachukua hatua.
"...Unapomwita kiongozi ni
dhaifu, maana yake unamlazimisha awe mkali, achukue hatua.
"Naona wengine wanahaingaika
sijui kufungua kesi....Lakini nasisitiza, Mimi ndio Spika, nasema mwaka mtu
hakanyagi hapa"
==>Mtazame hapa Ndugai akifunguka
zaidi.
No comments