Breaking News

MHE KIGWANGALA: TUNAMBUA MCHANGO WA WADAU KATIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

Related image
Serikali imesema inatambua mchongo wa wadau na mashirika mbalimbali katika kusaidia kuboresha na kupunguza changamoto zinayoikabili sekta ya afya nchini.
Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Mhe Dr. Hamis Kigwangala, Kaimu katibu mkuu wizara hiyo Bi. Otilia Gowele aliesema serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuahikikisha upatikanaji wa huduma bora za afya hususani kutoa elimu kwa wananchi juu ya afya ya uzazi.
Alisema serikali kwa kukishirikiana na wadau wengine ikiwepo shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA), kutoa elimu kwa wananchi kuhusu afya ya uzazi hili kukabiliana na ongezeko la watu pasipo tija.

Aidha Bi. Gowele aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa katika kila dola moja ambayo serikali inawekeza katika uzazi wa mpango mpaka dola sita zinaweza kuokoa shughuli nyingi za maendeleo zikiwemo kupunguza umasikini, elimu na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza.
Image result for Hashina  Begum unfpa tz
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Dr. Hashina  Begum alisema uwekezaji wa uzazi wa mpango ni kuwekeza katika afya pamoja na kuwekeza katika haki za wanawake duniani kote.

Alisema uzazi wa mpango ukizingatiwa Taifa litakuwa katika nafasi nzuri katika kuendelea uchumi na usawa wa kijinsia kufikia malengo 17  ya milenia ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani yanaadhimishwa sambamba na mkutano wa kimataifa unaoendelea jijini London juu ya malengo ya uzazi wa mpango kuelekea mwaka 2020, mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya “Uzazi wa Mpango kuwezesha watu na kuendeleza Mataifa”.

No comments