LADY JAY DEE AFUNGUKA HAYA MARA BAADA YA PROFESSOR JAY KUFUNGA NDOA
Msanii
wa Bongo, Lady Jaydee amempa pongezi za kutosha msanii mwenzie Professor Jay
kwa uamuzi aliyofikia wa kufunga ndoa.Weekend iliyopita siku ya Jumamosi Prof
Jay alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ‘Grace’ ambaye tayari
walishajaliwa mtoto mmoja.
Kuhusu
hilo Lady Jaydee amesema, “Kwanza nimpongeze Prof Jay kwa hatua aliyochukua, ni
hatua nzuri katika maisha kwa sababu kwanza ni kuzaliwa, pili ni kuoa au
kuolewa na ya tatu ni kufa, kwa hiyo hii ni harusi ya pili katika maisha yake
nimpongeze sana kwa uamuzi alioufikia,”.
Ameiambia
Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.“Nimtakie kila la kheri katika maisha yake
ya ndoa yenye furaha na mafanikio.
Professor
kama kaka yangu na kama rafiki yangu ni mambo mengi tumepitia pamoja, tumeweza
kusapotiana katika kazi na mambo mengine, kwa hiyo ni furaha kwangu, si kama
msanii mwenzake bali kama mwanafamilia,” ameeleza Lady Jaydee.
Professor
Jay na Lady Jaydee wamesharikiana katika nyimbo nyingi kama vile Kikao cha
Dharura, Bongo Dar es Salaam, Niamini na Joto Hasira.
No comments