EVERTON KUTUA NCHINI JULY 12 KUCHEZA NA GOR MAHIA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHv6eISxQeAEfjYzdphtyqCUc8lkqd17puRzOZpw51TfC02isWtqR1gFSKVE1yC5QDDJwPg7w_LsKSnAxFCiWYx7L3tM2rs5ZoumH8wYBXTcCR1AkCKj_YhwznT2zUWtjrutqy70xIx_Uk/s640/WhatsApp+Image+2017-07-11+at+13.55.17.jpeg)
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omary Singo
akizungumza kwa niaba ya Serikali katika kuupokea ugeni wa Timu ya Everton
wanaokuja kucheza Mchezo wa Kirafiki na Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13
mwaka huu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuKZ28Pv9U4DZD3xU_raEVye2Y0sEQ3Z1etoH-cUq8f2vvtPqSQdFx_W40d066J3R876zFZF0H9uSld1Z2o9ilj7z8FnxNYEwVtOWCWNa7cDVhBLKei1_FS-1wW9A7Tlthm3hpX8juyOIF/s640/WhatsApp+Image+2017-07-11+at+13.53.25.jpeg)
Mkurugenzi
wa SportPesa nchini, Abbas Talimba akifafanua jambo juu ya ujio wa Timu ya
Everton ya Uingereza July 12 mwaka.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsW5w9J1L_Kd1dmCpInHjyGFYwTJd56dFy-MNc1d3UBvpnbxJY_hxXamTE3FM4BW8E87H3QTxOVGRvN-EbkAWaHuq2AaRQZJ2K01FcOFdQUNfXNe3QBZKlMvoV0hFWfEsexsNwruryu1pO/s640/WhatsApp+Image+2017-07-11+at+13.57.13.jpeg)
Afisa Usalama wa TFF na FIFA, Inspekta Hasheem
Abdallah akifafanua kuhusu Ulinzi katika Mchezo huo utakaopigwa July 13 katika
Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgxi2ZV0uADiGxXdj9x8RIWGldJmzSQ9Wr0oWE37FO40KEFeHgia6MxSmr3qIh-ZrxHYa85WRY9aVvZBEtAxhWXJrw0pokD6zISP9hMhW_2B4UhC-Vsbt5IsU759nJIpmKinGfnv9K9hfL2/s640/WhatsApp+Image+2017-07-11+at+13.58.59.jpeg)
Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo - SELCOM,
Galusi Lunyeta akifafanua juu ya upatikanaji wa Tiketi siku ya Mchezo huo July
13. Picha na Anil Ricco, Globu ya Jamii.
Maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Gor Mahia
ya Kenya na Everton ya England, utakaofanyika Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, yamekamilika.
Tayari
Gor Mahia kutoka Kenya – Mabingwa wa SportPesa Super Six, imetua hapa Dar es
Salaam, Tanzania leo Jumanne, Julai 11, mwaka huu tayari kabisa kwa mchezo huo
utakaofanyika kuanzia saa 11.00 jioni.
Kwa
upande wa Everton, wao wataingia alfajili Julai 12, mwaka huu tayari kabisa
kuwakabili Gor Mahia katika mchezo ambao tayari tumetangaza kuwa Kiingilio
kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzunguko na Sh 8,000 kwa majukwaa ya watu maalum.
Timu
zote zitahudumiwa sawa kuanzia usafiri, hoteli na huduma za tiba hapa uwanjani
kuanzia siku ya mazoezi na siku ya mchezo wenyewe. Kila timu itapata dakika 45
mazoezi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Gor
Mahia watacheza leo Jumanne katika uwanja huu wa Taifa na Everton – zamu yao
itakuwa kesho Jumatano. Tumeweka muda huo kutokana na ushauri wa wataalamu wa
waliofanya marekebisho ya uwanja na namna bora wa kutunza uwanja.
Mama
Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanania, tunatarajia atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo, Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Michezo, Yussuf Singo amethibitisha hilo.
Kuhusu
viingilio, Ndugu zetu wa Selcom, tumekuwa nao pamoja na leo wanatuthibitishia
kuwa wamekwisha kuanza kuuza tiketi katika mtandao.
Ikumbukwe
tu tumeweka viingilio vya bei nafuu ili kuwapa Watanzania wengi fursa ya
kuingia uwanjani kushuhudia mechi hiyo ambayo timu zote ngeni, lakini kwa kuwa
Watanzania ni watu wa mpira, bila shaka watapata burudani murua na maridhawa
kabisa siku ya Alhamisi.
Ulinzi
umewekwa wa kutosha kabisa kwani kutakuwa na mbwa, farasi, magari ya kumwaga
maji yenye kuwasha mwili kwa wale ambao watabainika kuleta vurugu.
Jeshi
la Polisi na vyombo vingine vya usalama yakiwamo makampuni ya binafsi ya
ulinzi, wametuhakikishia kwamba watadhibiti kila aina ya vurugu zitakazotokana
na mashabiki wakorofi ambao wao huwaza vurugu kwa sababu zao mbalimbali.
Mchezo
utaanza saa 11.00 jioni na utarushwa hewani na vyombo mbalimbali vya habari vya
ndani kwa maana ya ninyi wenzetu kadhalika vya nje ya mipaka ya Tanzania.
TFF
wametuambia kwamba wameratibu vema kabisa mchezo huo katika maeneo ya Itifaki,
ufundi na vyombo vya habari.
Kuhusu
ufundi uwanjani ni kwamba Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Israel Mujuni Nkongo wa
Dar es Salaam, ambaye atakuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ferdinand Chacha
wa Mwanza – mshika kibendera wa kwanza na Frank Komba ambaye atakuwa mshika
kibendera wa Pili.
Mwamuzi
wa akiba atakuwa ni Elly Sasii. Waamuzi wote hao ni wale wa beji za FIFA.
Kamisha wa mchezo huo atakuwa ni Michael Richard Wambura wa Dar es Salaam.
No comments