CHADEMA YATANGAZA OPERESHENI 'ONDOA MSALITI'
Dar es
Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni
maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua
mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).
Operesheni
hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim
Seif.
Akizungumza
leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kanda ya
Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya
upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini
ya mwavuli wa Ukawa.
Kubenea
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF
ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama,
bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni
msaliti.
"Sisi
kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti
Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi
Buguruni, "amesema Kubenea.
Kadhalika
amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote
za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na
Profesa Lipumba.
Chanzo-Mwananchi
No comments