UNFPA: Wanawake Mil 214 Awatumii Njia Za Uzazi Wa Mpango.
Wanawake takribani milioni 214 waishio katika
mazingira hatarishi kutoka nchi zinazoendelea duniani wanakadiriwa kukosa
njia bora za uzazi wa mpango.
Kaimu
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu (UNFPA) Dr. Hashina Begum amewaambia
waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM kuwa jumla ya wanawake kutoka mataifa
69 duniani wamekuwa wakikosa fursa ya afya ya uzazi.
Dr.Begum amebainisha kuwa ili
kukuza uchumi na kuleta maendeleo duniani ni lazima kukabiliana na changamoto
hiyo inayowakumba zaidi wanawake masikini pamoja na wakimbizi.
Aidha Dr. Begum amesema kuwa ni vema jamii kutoa fursa kwa
wanawake kupewa elimu hasa ya afya ya uzazi wa mpango kwakuwa wanawake
wanaotumia njia ya uzazi wa mpango wanapunguza vifo kwa asilimia 30 na kwa
watoto kwa asilimia 12 katika utekelezaji wa lengo la UNFPA ifikapo mwaka 2030.
Nae Dr. Cosmas Swai kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia
wazee na watoto amesema kuwa wizara ya afya kwa kushirikiana na UNFPA na wadau
wengine wa afya wamejipanga vema katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu
duniani ambayo Itafanyika tarehe 11 -12julai,2017 katika viwanja vya Mwembe
yanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Afya Dk.Khamis
Kigwangala.
Kwa
upande wake Afisa mawasiliano na utetezi kutoka Chama cha uzazi na malezi bora
Tanzania (UMATI) Bi Josephine Mugishagwe ameitaka jamii kujitokeza ili kupata huduma za
upimaji wa hiari wa VVU,matumizi sahihi ya kondom, Afya ya saratani ya shingo
ya uzazi,Huduma ya uzazi wa mpango ambazo zitatolewa bure.
Kaulimbiu ya
mwaka 2017 ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani ni “Uzazi wa Mpango kuwezesha watu na kuendeleza
Mataifa
No comments