WAKAZI WA MANISPAA YA TEMEKE MWEMBE YANGA WAELEZEA ADHA YA DAMPO KARIBU NA MAKAZI
Wakazi wa manispaa ya temeke mwembe yanga
wamelalamikia kero kubwa wanazopata kutokana na dampo la uchafu ambalo limekuwa
likisababisha kero kubwa kwao na kuwa tishio dhidi ya magonjwa ya milipuko
ikiwemo kipindupindu.
Akizungumzia kero hiyo jijini Dar es
salaam mkazi wa Temeke Shekh Jamal Twahir amesema kuwa tatizo hilo limekuwa
sugu kwakuwa dampo hilo lipo maeneo ya makazi ya watu ambapo jumla ya kata kumi
na nne zote zinaleta na kumwaga taka hapo katika kata ya Sandali na Tandika na
kusema kuwa jambo linahatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Kwa upande wake mwinjilisti Cecil Simbaulanga ambae ni mkazi wa eneo hilo amesema
kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakipata shida kutokana na uchafu wa dampo
hilo ambalo limekuwa linarundikana taka tofauti na wilaya nyinginezo.
Simbaulanga ameiomba serikali kuhamisha dampo
hilo katika upande wa uwanja usiokuwa na makazi ya watu ili wakazi wa eneo hilo
wasiendelee kuathirika na taka hizo ambazo ni tishio kwa jamii.
Nae Juma Uweso amesema uwanja huu
umekuwa ukitumika kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, michezo lakini cha
kushangaza ni kwamba uwanja huo huo umekuwa dampo lisilozolewa
uchafu pindi shughuli za kitaifa zisipokuwepo.
Kero za dampo hilo zimekuwa
changamoto kubwa kwa wakazi waishio kata ya sandari na tandika kwa kipindi
kirefu sasa.
Sikilza mmoja ya wakazi wa emeo hilo akielezea==>>
No comments