KAULI YA MHE LOWASSA BAADA YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI, AKUKABIDHIWA RIPOTI YA PILI YA MCHANGA WA MADINI
“Nimpongeze sana Mhe Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi na
hatua ambazo amechukua kuhusu jambo hili, na hasa pale anapowashirikisha
wananchi, ni jambo muhimu sana.
Maneno
hayo yalisema jana na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la mchanga wa madini
(makinikia) ambalo limeonyesha kuwa Tanzania impoteza zaidi ya trilioni 100
tangu mwaka 1998 hadi Machi mwaka 2017.
Lowassa
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alisema anampongeza Rais Magufuli
kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA kwani kipindi anazunguka kuomba kura
kwa wananchi alipopita maeneo yenye madini aliyazungumza haya yanayotekelezwa
leo.
“Nampongeza
kwa kutekeleza yale maamuzi ambayo ni ya UKAWA. Nilipokuwa kwenye kampeni ya
kuomba kura, hata pale Geita, nilieleza jambo hilo, nikasema hivyo hivyo
alivyosema yeye kwamba nikiingia madarakani nitaunda tume ya kuchunguza jambo
hili ili mtanzania awe ndiye anapata sehemu kubwa ya faida kuliko mgeni.”
Aidha,
Lowassa amesema kuwa, ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na hata yeye
alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa na na kuzungumza,
lakini jambo gumu lilikuwa ni kamba, mikataba ukishaiweka saini inakuwa migumu
sana kubadilisha.
Lowassa
alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo
mirahaba lakini haikutosha.
“Matumaini
yangu ‘figure’ (namba) hizo ni za kweli, kama ni za kweli, tumeliwa kweli
kweli,” alisema Lowassa alipokuwa akizungumzia mahesabu yaliyowasilishwa katika
ripoti za uchunguzi kuhusu kiasi cha fedha ambazo Tanzania imepoteza
No comments