SHEIKH PONDA: AMEITAKA SERIKALI PAMOJA NA BUNGE KUUNDA KIKOSI KUCHUNGUZA NA KUMALIZA MAUAJI YANAYOENDELEA MKOANI PWANI.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa
Dar es Salaam.
Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa ameitaka Serikali
pamoja na Bunge kuunda kikosi cha watu kitakachoweza kusaidia kumaliza kabisa
mauaji yanayoendelea kuripotiwa mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya
swala ya eid katika msikiti wa Magomeni kichangani alisema kitendo cha
kuviachia Vyombo vya usalama peke yao bila ushirikiano na watu wengine hawawezi
kumaliza tatizo hilo kwa haraka.
“Katika kipindi cha
Ramadhani tumeshuhudia viongonzi wengine wanaendelea kuuwawa kiasi kwamba serikali
inatakiwa kuongeza nguvu ya kutosha ilikutokomeza tatizo hilo” alisema Ponda
Alisema wabunge nao
wanatakiwa kulitilia mkazo jambo hilo pamoja na kwenda kuongea na wananchi wa
maeneo hayo na kuweza kujua chanzo cha tatizo juu ya mauaji hayo.
Sheikh Ponda Aliongeza
huenda wananchi wa maeneo hayo wanaogopa kuibua watu hao kutokana na njia
inayotumiwa na Polisi ya kuwahoji wananchi hao na kuwakamata imekuwani ya
kimabavu.
“Wananchi hao kwa sasa
wameonekana wakiishi katika maisha ya hofu kiasi kwamba wanajamii wanatakiwa
kuleta ushirikiano kwa jeshi la polisi ilikumaliza mauaji hayo.”alisema Ponda
Sheikh Rajabu Katimba
Kwa upande wake Msemaji
wa Taasisi hiyo, Sheikh Rajabu Katimba alisema kuwepo kwa kikosi cha
watu saidiaana na jeshi la polisi kutaweza kusaidia kujua chimbuko
la tatizo hilo.
Alisema wanaendelea
kulaani vitendo hivyo vikundi hivyo vinavyo angamiza maisha ya wanadamu pasipo
kujua wanahitaji vitu ganizaidi.
“Kibaya zaidi kinacho
tusha ngaza zaidi kwanini mauaji hayo yanaangamiza watu wa jamii moja wizara
husika inatakiwa kujua chanzo chake”. alisema Katimba
Aidha shekh katimba alishauri
kuwa kama matukio hayo yanahushisha masuala ya kisiasa Serikali pamoja na bunge
wanatakiwa kulitafutia ufumbuzi wa haraka.
No comments