Breaking News

MADEREVA DAR-BAGAMOYO WAMEIOMBA MANISPAA YA KINONDONI KUKARABATI KITUO CHA TEGETA NYUKI. DIWANI ATOA NENO…

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Dar–Bagamoyo, Bw. Cliff Ngomuo, akifafanua kuhusu changamoto mbalimbali wanazo kabiliana nazo katika kituo cha basi cha tegeta nyuki.

Dar es salaam:
Madereva wanaosafirisha abiria kutoka stendi ya tegeta nyuki Dar kwenda Bagamoyo wameiomba manipsaa ya kinondoni kukarabati miundombinu ya kituo hicho kwani imekuwa kero kubwa kutokana na miundombinu yake kuwa katika hali mbaya.

Akizungunza na waandishi wa habari kituoni hapo mwenyekiti wa chama cha madereva Dar–Bagamoyo, Bw. Cliff Ngomuo alisema kufatia halmashauri kuwataka kuanza kutumia kituo hicho badala ya makumbusho kero kubwa ni miundombinu ya kituo hicho hususani barabara zinazoingia na kutoka kituoni hapo.
Alisema wao awana tatizo na uhamuzi wa halmashauri ambao umewataka kuanza kuishia kituo cha tegeta nyuki kama leseni zao zinavyoonyesha, bali mindombinu kituo hicho jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao na watumiaji wa usafiri huo hususani usiku kutokana na kutokuwepo taa.
Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani wa wilaya ya kinondoni,ACP Theopista Mallya akifafanua jambo mbele ya madereva na makonda wanaosafirisha abiria kati ya Dar-Bagamoyo kuhusu leseni zao za kutoa huduma na hatua ya kuwaondoa katika kituo cha makumbusho na kuishia tegeta nyuki.
ACP Theopista Mallya, alisema kwa mujibu wa leseni zao wanatakiwa kuishia katika kituo hicho ila swala la wao kuwa wanaishia makumbusho lilikuwa ni la mda tu hivyo kuwasisitiza kufata sheria na utaratibu kama leseni zao zinavyowaelekeza.
“Kwa mujibu wa leseni zenu mnatakiwa kuishia tegeta nyuki kwahiyo yeyote atakayekaidi agizo tayali atakuwa amevunja sheria sambamba na kukiuka matakwa ya leseni zenu zinavyosema” Alisema. 
Diwani wa kunduchi Mhe. Michael Urio

Akizungumzia changamoto hizo diwani wa kunduchi Mhe. Michael Urio alisema ofisi yake tayali imeshaanza kuzishughulikia changamoto za kituo hicho kwa kuomba fedha Bil 3 katika bajeti hii kwa ajili ya kuzikarabati barabara zinazingia na kutoka kituoni hapo kwa kiwango cha lami.
Alisema pia ofisi yake tayali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuchonga barabara za kuingia na kutoka kituoni hapo kufatia mabasi kuanza kutumia kituo hicho alkini kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni zoezi hilo amelisitisha mpaka mvua zitakapoacha.
Bw. Urio aliongeza kuwa pia ofisi yake imeshaleta wataalam hili kusanifu eneo hilo kuweza kuweka taa kituoni hapo jambo ambalo limeshaanza kulitelekelezwa.   

Mwonekeno wa kituo cha mabasi cha tegeta nyuki.


No comments