MEYA WA UBUNGO BONIFACE JACOB, ATOA UFAFANUZI JUU YA SAKATA LA KUMPATIA JINA LA MTAA VICTOR WANYAMA,AFUNGUKA HATA MBWANA SAMATA AKIJA UBUNGO TUTAMPATIA MTAA.
Asalaam ayelkum Watanzania,
Tangu jana kutoka habari ya
kumpatia Jina la mtaa VICTOR WANYAMA, kata ya Ubungo na mtaa wa Ubungo N.H.C,
nimeona kumekuwa na mijadala juu ya hilo, nimeamua nitoe somo juu ya jambo hilo
kuepuka kuposhwa na wachambuzi uchwara.
Sheria namba 8 ya mwaka 1982 (sura
namba 288) na sheria namba 6 ya mwaka 1999 ,ndiyo inayotoa mamla kwa serikali
za mitaa kutunga na kutoa majina ya barabara za ndani ya halmashauri na
barabara za mitaani.
*Soma sheria namba 8 ya mwaka 1982(sasa inaitwa sura 288)
kifungu cha 55(1)j-to name or re name,where necessary,all streets(such names to
be affixed in conspicuous places),and to cause the buildings in such streets to
be numbered;*
TARATIBU ZA KUTOA MAJINA YA MTAA
Majina ya mtaa yana ngazi kuu
tatu ya upatikanaji na upachikaji wa majina, katika mamlaka za serikali za
mtaa, majina huanzia kwenye kamati za mtaa ndani ya serikali ya mtaa kwa
mamlaka za miji na majiji kisha mapendekezo hayo huenda kamati ya mipango miji
na mazingira ngazi ya wilaya na hutoka na azimio la kukubaliwa kwa jina
pendekezwa.
Na baadae baraza la madiwani
hupokea na kupitisha taarifa ya kamati ya mipango na mazingira.
NJIA ZA KUOENDEKEZA MAJINA YA MTAA
1. kwa viongozi wa kuu wa nchi
kuleta mapendekezo ya kubadili au kutunga jina la barabara kama wana mgeni wa kitaifa.
2. Kwa mtu kujitolea kuwa mlezi
wa barabara mtaani, ipitike vizuri basi huweza pewa jina lake.
3. kwa njia ya asili ya
kufuatisha majina ya watu maarufu katika mtaa, mara nyingi hawa huwa hawaombi
bali upendekezwa na wananchi.
4. kwa kikao cha kamati ya mtaa
au wananchi kukaa na kupendekeza jina mara baada ya kuona wanasababu zao hapo
mtaani kwao.
5. kwa kutoa kwa Heshima ya mgeni
aliyetembelea mtaani kwao kama kumbukumbu ya mtaa husika na viongozi wake.
*SWALI*
*kwa nini Victor wanyama na siyo
samata?*
*JIBU*
Mimi nilipokea ujumbe wa viongozi
wa UBUNGO FOOTBALL ASSOCIATION (UFA) mapendekezo ya kuja mtaani kwangu kata ya
ubungo siku ya jumamosi ya tarehe 24 June ya kwamba nitapokea ugeni wa
wachezaji wa wili kuja mtaani kwetu, wageni waliotarajiwa kupokelewa ni Mbwana
Samata wa Tanzania na Victor Wanyama (Kenya) kwa bahati mbaya alikuja mmoja
ambaye ni Victor wanyama,ndiyo maana tukio linaonekana ni yeye tu amekabidhiwa
jina la mtaa.
*SWALI*
Je Mbwana Samata akija ubungo mtampatia jina la mtaa*
*JIBU*
Tayari kamati ya mtaa ubungo
N.H.C walisha kaa kikao na kukubali kuwapatia wachezaji hawa wa ulaya barabara
mbili tofauti, ya Mbwana Samata zamani ilikuwa BENKI STREET (mita 800) na
Victor Wanyama zamani iliitwa VIWANDANI STREET (mita 270) ambapo kwenye kikao
chao cha mtaa mimi si mjumbe ila nilipendezwa na Idea ya mtaa wa N.H.C na
kuwapa full support.
*SWALI*
*Kwa nini Victor Wanyama tu na
siyo wanamichezo wengine maarufu wa zamani*
*JIBU*
Mimi ni kiongozi wa ngazi ya
wilaya Ubungo na siyo kiongozi wa Kitaifa au Waziri wa michezo hivyo ninayo
mamlaka ya kumsaidia mtu kupatiwa jina la mtaa katika ngazi yangu tu ili hao
mnao wataja wapate mtaa huku halmashauri ya Ubungo tunawakaribisha waje wapokee
barabara za kuzilea na kuzihudumia kama Victor Wanyama.
Pili, tulipendezwa na swala la
victor kuja mtaani kwetu kutia hamasa vijana wetu wanaochezea ligi ya Ndondo
cup, ligi yenye timu zisizo na madaraja rasmi TFF, hasa kipindi hiki cha
mapumziko yake binafsi achilia mbali na utajiri wake, lakini akae kutimuliwa
vumbi kiwanja cha kinesi, na kuwapa hali na mori vijana wa ubungo wenye ndoto
kama yake ya kuchezea ligi za kulipwa ulaya.
Tunatamani wengine waje tuwape
hadhi na heshima sawa na ya Victor Aliyo wapatia vijana wa ubungo, sembuse
kuita jina la mtaa, tena wenye vumbi.
*Je na wewe unataka jina la mtaa
wako?*
Ni rahisi sana chukua jukumu la
kuhudumia moja ya barabara za mtaani kwako kisha nenda serikali ya mtaa
unapoishi, waombe wakukabidhi rasmi barabara ya mtaa au fanya jambo lenye
kuletea heshima na kuitangaza vema ndani na nje ya nchi halmashauri yetu ya
Ubungo.
BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
No comments