MAMA SAMIA AZINDUA JUMUIYA YA WATOA HUDUMA ZA MAFUTA NA GESI TANZANIA (ATOGS)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa
Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana
na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana
Jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha
kitabu cha picha alichokabidhiwa na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji
(kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa
Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji alipokuwa
akisaini katika kitabu cha picha alichomkabidhi Makamu wa Rais wakati wa hafla
ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na
Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta
na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu
malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya
hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi
milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)
jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na
Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles
Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa
Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi
mstaafu Balozi Ombeni Sefue(kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na
Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw.
Abdulsamad Abdulrahim.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi
Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na
uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Picha
na: Frank Shija - MAELEZO
No comments