SERIKALI IMEOMBWA KUWAANGALIA WAJANE KWA JICHO PEVU
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9FeUnJ9SyEOFF5Y6iGJUM9MF4e4fOhs7UdEjM765MfUTpUE3A_UC0iGj8D9JkWnUhwiHHl_VJccor5sQEo2UEhzxTmUaOgXsre87t2Nh9JEVWL5ebB30gYuPKxzN06ONgs3harXMSLuDd/s640/20170624_182345.jpg)
Mtumishi wa Chuo cha Imam Swadiq
(a.s) Bi Fatma Mwiru akiwasilisha mada yake mbele ya Wanawake Wajane
waliohudhuria katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uomgozi wa
Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, Kigogo Post jijini Dar es salaam.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8OiYXG_A5-_VXjLmR8-Tr13dnVrNguY5B2zspg-62MWVl-tY3GIlCksb6ioqh5k7BQLDr-A3p5D8AgPddeWLco-aOuAIdg-U92llYyS9JUOl4l20uhuW5-P2aoGgQgu5bJkOrHUjUzIWO/s640/20170624_182302.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja63gnMchw7CojM0_J75mCDnohlxWuMpOZ0evUks6Lfm-RHLLmwBjF6s4yKvIyPiOH0bDpmK9CVq6L_lPEtSvtWG8E-LNe3N5jbFAHcRPBNyDFjl10NBZAfRT8hHq7d4yWSWxCGGsCdQss/s640/20170624_182403.jpg)
Baadhi ya Wanawake Wajane walioshiriki katika hafla
ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam
Swadiq, jana Kigogo-Post Jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Mwenyekiti Msaidizi wa
Chama cha Wajane Tanzania Wilaya ya Ubungo Dar es salaam Mh Josephine Chale
amemwomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kuwaangalia
Wajane kwa jicho la kipekee ili aone namna gani anaweza kuwasaidia katika Nyanja ya
sheria ambayo itazuia wajane kuonewa kwa kudhulumiwa haki zao
Chale amewaomba Wajane
nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa Mjane haina maana ndio mwisho wa
Maisha,kwani haliya kuwa maisha yanaendelea
Aidha Chale ameushukuru
Uongozi wa Msjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kuweza kuwaalika Wajane katika
futari ya pamoja ili Wajane wajisikie kwamba na wenyewe wanatakiwa katika
jamii, ili wasijitenge kama vile kwamba wamefiwa basi ndio maisha yamefika mwisho.
Hayo alisema jana katika
halfa ya futari ya pamoja na Wajane,iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir
na Chuo cha Imam Swadiq Vilivyopo Kigogo Post Dar es salaam.
“Napenda tena kuwashukuru
Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kwa kutualika sisi wajane,
tumepata faraja kubwa sana, kwani na sisi tutaenda kufanya kama wanaofanya
wenzetu ili tuwape amani wajane.Tunashukuru sana sana,tunamuomba Mungu awape
Moyo wa upendo, awape riziki na awape maisha marefu.”
Kwa upande wake Mtumishi
wa Imam Swadiq Bi.Zaynab Ndete alisema lengo la hafla hii ya Futari ya Pamoja
na Wajane, ni Tumewaalika wanawake Wajane kutoka Wilaya mbalimbali
za Mkoa wa Dar es salaam, lengo kubwa ni kuzungumza nao na kuwapatia muongozo
wa Kisheria, hususani zinazowahusu wao baada ya kufiwa na waume zao.
“Kwa kweli swala ya Ujane
ni swala zito ni swala gumu, kwasababu ni swala linalomuhusu mwanamke, kama
tunavyoangalia katika jamii yetu ya Kitanzania wajane wengi wanapokuwa wametoza
wame zao, wanakuwa ni watu ambao wanakuwa katika matatizo makubwa sana,
miongoni mwa matatizo wanayokumbananayo ni kutengwa au kunyanyapaliwa na
familia ya mume ,kunyang’anywa haki zao za msingi, kunyang’anywa mali zao
ambazo wameachiwa kama urithi na wame zao” alisema Ndete
“Sisi Uongozi wa Masjid
Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq tumewaita hapa kwanza kuwasaidia waweze
kuzifahamu haki zao, wamama wajane hawatakiwi wawe wanyonge pale wanapoondokewa
na wame zao,kuondokewa na mume ni jambo Mwenyezimungu (swt) ameliandika kuwa ni
lalazima kwani anaweza kuondoka Mume au Mke” aliongeza Ndete.
“Dini ya Kiislam
imesimama kidete juu ya kuwatetea wanawake wajane, kwani ukiwa mjane unahaki ya
Kuishi kama wengine,anahaki ya kuwa na mali,unahaki ya kuwa Kiongozi,unahaki ya
kuwa Bosi, anahaki kuwana amani na upendo, anahaki ya kuwa Muajiriwa, anahaki
ya kuolewa na Mwanaume mwingine,anahaki ya kumiliki” alisisitiza
Hata hivyo Mtumishi Ndete
aliwaomba Wanawake wajane wasiwe wanyonge na wasimame kidete kuweza kusimamia
malezi ya familia zao kwani jukumu la kuwalea watoto aliokuwachia mumewe iko
mikononi mwako.
No comments