MAHAKAMANI KWA KUMUINGIZA MTU MWEUSI KWENYE JENEZA AFRIKA KUSINI
![Willem Oosthuizen na Theo Jackson](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/18518/production/_96680699_d63fd1bc-09d8-4ead-ab7c-3ca96af434a7.jpg)
Wakulima
wawili weupe watafikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini , baada ya kutuhumiwa
kuwa walimsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku
wakitishia kumwagia mafuta ya petroli na kumteketeza moto, akiwa hai.
Wakati Victor Mlotshwa alipokataa,
wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.
![Victor Mlotshwa](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/29D4/production/_96680701_60b00a6d-716e-4388-838b-08fb6f88bb57.jpg)
Washtakiwa hao Willem Oosthuizen
na Theo Jackson, walikamatwa mwezi Novemba mwaka jana, baada ya video ya
kitendo hicho kilipowekwa mitandaoni.
Walisema kuwa, Bwana Mlotshwa
alipitia kwenye shamba lao liliko katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na
idhini, na walikuwa wakimuadhibu.
Katika kusikizwa kwa kesi hiyo
awali, jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa wakatili na waliojaa
tabia za ubaguzi wa rangi.
No comments