KAULI YA RAIS MAGUFULI KWA WATUMISHI WA UMMA
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo wakati akizindua Mfumo wa serikali wa
ukusanyaji kodi kwa njia ya Kieletroniki amewachana baadhi ya watumishi wake
akisema wamekuwa wakiwaza mambo makubwa ambayo wanashindwa hata kuyatimiza.
Rais Magufuli amesema
kuwa watumishi wengi wamekuwa si wabunifu katika kuangalia vyazo vya mapato
ambavyo vinaweza kusaidia serikali kuingiza pesa nyingi lakini wao wamekuwa
wakiwaza kuongeza bei ya pombe tu na kuacha vitu vingine ambavyo vingeweza
kuongeza mapato kwa serikali kwa njia nyingine nzuri.
"Saizi watu
wanahangaika na Machinga wakati tungeweza kutengeneza vitambulisho vya
wamachinga na kila kimoja tukauza labda elfu kumi, Machinga akinunua
kitambulisho hicho anatambulika na serikali na kinaeleza kuwa anapaswa kuwa
wapi, je, ni shilingi ngapi tungezipata hapo kwa idadi wa wamachinga waliopo
nchi nzima? Lakini watu wetu wao wanawaza kuongeza bei ya pombe tu, yaani tuna
watu wa uchumi wengi lakini sijui hata wanafikiria nini " alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais
Magufuli alisema hata tabia ya watu kukwepa kulipa kodi inasababishwa na
mipango mibovu akitolea mfano kuwekwa bei juu ya kodi ya majengo jambo ambalo
linafanya watu wengine kushindwa kulipa kodi hiyo na serikali kupoteza mapato.
"Watu wetu hawa
hata kwenye kodi ya majengo unakuta wameweka mtu alipe milioni mbili sasa hizo
pesa wananchi wanazipata wapi? Ndiyo maana wanakwepa kodi sababu hawana pesa
hizo lakini kama wangeweka labda elfu kumi, ishirini mpaka hamsini halafu wenye
maghorofa labda laki mbili ungeona kila mtu angekimbilia yeye mwenyewe kulipa
kodi, kwa nyumba zote zilizopo Tanzania tungepata shilingi ngapi? Lakini
wameweka pesa kubwa na hawazipati sababu watu hawalipi hawana hizo pesa"
alisisitiza Rais Magufuli
Katika hatua ya
mwisho Rais Magufuli aliyaomba makampuni ya simu nchini yawe mfano wa kuingwa
na ikiwezekana yawe ya kwanza kabisa kujiunga katika mfumo huu mpya wa
ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kieletroniki kwani mfumo huu una manufaa kwa
wawekezaji na Watanzania kwa ujumla.
No comments