NSSF YAPUNGUZA SIKU ZA KULIPA MAFAO KUTOKA 60 HADI 30
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dodoma Machi 17, 2025, ambapo ameelezea mafanikio lukuki ya mfuko huo, kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Maafisa wa NSSF wakijadiliana jambo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo
Dodoma - Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kuimarika, ambapo thamani yake imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 4.28, Februari 2021 hadi Shilingi Bilioni 9, Februari 2025, sawa na ongezeko la asilimia 92.
Akizungumza leo Machi 17, 2025, Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema ukuaji huo umetokana na kuongezeka kwa wanachama, mapato yatokanayo na michango, pamoja na thamani ya vitegauchumi vya mfuko.
Kwa mujibu wa Mshomba, NSSF imeandikisha wanachama wapya 1,052,176 kati ya Machi 2021 na Februari 2025, huku michango ikiongezeka kutoka Shilingi Bilioni 1,131.92 mwaka 2021 hadi Shilingi Bilioni 2,153.13 mwaka 2025, ongezeko la asilimia 90.
Ameeleza kuwa, miradi mikubwa ya uwekezaji, kama vile Bwawa la Mwalimu Nyerere, Mgodi wa Nyanzaga, Kiwanda cha mbolea Intracom, na Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), imechochea ukuaji wa mfuko huo.
“Michango inayokusanywa imefikia Sh bilioni 6,994.52, ikionyesha uimara wa mfuko na kuleta uhakika wa mafao kwa wanachama,” amesema Mshomba.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji, jambo ambalo limechangia ukuaji wa sekta mbalimbali, ikiwemo viwanda, kilimo na utalii
Post Comment
No comments