OMO: WENYE MAMLAKA WENGI HAWATENDI HAKI KWA WANAOWAONGOZA
Mwenyekiti wa ACT wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Ndugu othman Masoud akizungumza katika iftar ya pamoja na viongozi wa siasa, dini, serikali, jamii na wanahabari na wananchi mbalimbali Machi 12, 2025 katika Ukumbi wa Hotel ya Peacok Hotel Jijini Dar salaam.
Kiongozi wa Chama Mstaafu, Ndugu Zitto kabwe akisalimiana na Sheikh Ponda katika Iftar iliyoandaliwa na Mwenyekiti Taifa wa ACTwazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndugu othman Masoud katika Hoteli ya Peacock, Dar es salaam jana tarehe 12 Machi 2025.
Sheikh Issa Ponda akizungumza katika iftar iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT wazalendo Machi 12, 2025 katika Ukumbi wa Hotel ya Peacok Hotel Jijini Dar salaam.
Askofu Emmaus Mwamakula akifafanua jambo wakati akizungumza katika iftar iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT wazalendo Machi 12, 2025 katika Ukumbi wa Hotel ya Peacok Hotel Jijini Dar salaam.
Mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo Taifa, Ndugu othman Masoud akisalimiana na Askofu Emmaus Mwamakula katika iftar aliyoiandaa jana Machi 12, 2025 katika Ukumbi wa Hoteli ya Peacock Jijini Dar es salaam.
Dar es salaam - Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Ndg Othman Masoud Othman, amesema nchi ya Tanzania inaharibikiwa kwa kuwa viongozi wengi wenye mamlaka ya maamuzi, hawawatendei haki watu wanaowaongoza.
Aidha Ndugu Othman ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,amesema kiongozi yeyote atakayesimama kwa ajili ya haki ya wananchi wake ataishi kwa amani maisha yake yote bila ya kuwa na hofu.
Mhe. Othman ametoa kauli hiyo jana jijini Dar esSalaam, wakati akiwashukuru waumini wa dini ya kiislam, viongozi wa Serikali, Masheikh na Maaskofu waliohudhuria katika futari aliyowaandalia katika hoteli ya Peacock.
Amesema ni heri kuwaachia wahalifu 100 wenye makosa kuliko kudhulumu haki ya mtu mmoja asiyekuwa na hatia na kuwataka viongozzi wa Serikali kujihadhari na watu wanaowazunguka kwa kuwa wengi wanawapotosha kutenda yasiyofaa.
Katika hafla hiyo ya futari viongozi mbali mbali wa dini na Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri Tanzania walipata nafasi ya kutuma salamu zao ambapo Sheikh Ponda Issa Ponda,alimueleza Ndg Othman kuwa viongozi walio madarakani wameshindwa kuangalia sheria zinazokandamiza haki za binadamu hasa ucheleweshwaji haki mahakamani.
Sheikh Ponda alisema, kuna Watanzania wapo magerezani kwa zaidi ya miaka 10 lakini serikali imeshindwa kuthibitisha madai yao kwa maelezo kuwa uchunguzi unaendelea na kutolea mfano Masheikh waliokamatwa hivi karibuni kuwa wamekaa gerezani miaka 10 na wiki iliyopita waliachiwa huru na baada ya siku moja Serikali imewakamata na kuwafungulia mashitaka mapya wakati yale ya kwanza wameshindwa kuyathibitisha.
Kwa Upande wake Askofu Emaus Bandekile Mwamakula, aliwataka viongozi wajitathmini kama ibada hii ya kufunga wanaitendea haki, ikiwa matendo ya watu kutekwa,Hhaki za raia kuzidi kuminywa na watu kuendelea kuishi katika hofu hakujapatiwa ufumbuzi.
No comments