Breaking News

DC KISARE: TUUNGE MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI ZA KULETA MAENDELEO, KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe Makori Kisare akizungumza mara baada ya kupokea mwenge wa uhuru jijini dar es salaam..
Kiongozi wa mbio za mwenge Amour Hamad Amour akizindua moja ya miradi ya maendeleo iliyozinduliwa katika wilaya ya ubungo jijini da es salaam.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe Makori Kisare ameupokea rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka kwa  mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh.Hapi mara baada ya Mwenge kumaliza ziara yake katika wilaya ya kinondoni.

Mhe Kisare ameishukuru serikali ya awamu tano chini ya Mhe Dkt. John Pombe  Magufuli kwa juhudi anazofanya za kuleta maendeleo kwa Taifa sambamba na kukuza uchumi kuelekea Tanzania ya viwanda.

Akizungumzia ujio wa mwenge Wa Uhuru mhe Kisare alisema katika wilaya hiyo umekagua na kuzindua miradi mbalimbali iliyopo wilaya Ubungo kama kituo cha Huduma na  Tiba kwa wagonjwa waishio na Vvu na Ukimwi kilichopo Mbezi ambacho kinatarajiwa kuhudumia watu wapatao elfu kumi mradi huo uliibuliwa na idara ya Afya ya manispaa ya Ubungo.

Mradi huo umegharimu shilingi milioni 155 ambazo zimetolewa kwa msaada wa wafadhili wa Management & Development for Health (MDC).

Mbali na hayo kiongozi wa mbio  za Mwenge alizindua mradi wa madarasa nane yaliyopo katika shule ya Msingi iitwayo Malamba mawili iliyopo katika manispaa hiyo ambayo yamejengwa kwa fedha za serikali zilizogharimu shilingi 136,000,000.

Maeneo mengine yaliyotembelewa na kuwekwa jiwe la msingi ni kituo cha polisi kati Gogoni kilichopo Kibamba ambacho kinakusudiwa kuwa na jumla ya vyumba 13 wananchi wakiwa wamechangia shilingi 53,000,000 na Nssf wamechangia  50,000,000 jumla ikiwa shilingi 103,000,000.

Akizungumza kiongozi wa mbio  za Mwenge Amour Hamad Amour katika uzinduzi wa kituo cha mawasiliano cha mabasi  kiitwacho simu 2000 na kituo cha polisi  amewataka madereva watumiao kituo hicho kuzingatia idadi ya upakiaji abiria.

Aidha Amour amewataka madereva hao kujiepusha na ulevi pamoja na utumiaji wa mirungi.

Kituo hicho cha mabasi kina uwezo wa kuhudumia mabasi 560 na bajaji kimejengwa kwa pesa za mapato na kugharimu shilingi 2,376,647,991.89.

Mwenge wa uhuru umehitimisha ziara yake mburahati  ambapo umetembelea kituo cha zahanati mburahati ambacho kina uwezo wa kuhudumia watu 30,000 waliopo huko na maeneo ya Barafu utagharimu shilingi   84,000,000.00.

No comments