MAREKANI YAANZA KUJIPANGA KUKABILIANA NA MAKOMBORA YA KOREA KASKAZINI
Marekani
imesema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jaribio lake la kwanza la
mtambo wa kutungua makombora ya nyuklia ya masafa marefu.
Mtambo
huo wa ardhini umefungwa katika kambi ya kijeshi iliyopo Califonia kwaajili ya
kujihami na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa na maadui zake ikiwemo Korea
Kaskazini.
Aidha,
Pentagon imesema kuwa jaribio hilo limefanyika baada ya Korea Kaskazini kufanya
majaribio yake ya makombora tisa ya masafa marefu mwaka huu hivyo kutishia
usalama wa nchi hiyo.
“Mfumo
huu ni mhimu sana kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni uthibitisho
mkubwa kwamba tuna uwezo wa hali ya juu wa kujilinda na kutetea usalama wa raia
wetu,” amesema Mkurugenzi wa kitengo cha ulinzi wa makombora, Admirali Jim
Syring.
No comments