RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA TANZANIA NA UGANDA KUjadili MAENDELEO YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha
pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau
kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima
nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano
huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam JANA
Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini
pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert
(CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja
na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na
kukubaliana kwamba rasimu ya makubaliano
rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha
wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi
kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.
No comments