UNESCO, CHUO CHA BEIJING NORMAL NA WIZARA YA ELIMU WAZINDUA MRADI WA KUWEZESHA WASICHANA
Dodoma - Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha BNU (Beijing Normal University) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wamezindua mradi utakaowezesha wasichana na wanawake katika nyanja za sayansi, uhandisi na hisabatii.
Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 14, 2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Elimu Msingi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Abdul Maulid Mnonya aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo amesema uzinduzi huo utachochea kupata wataalam katika kukuza maeneo ya sayansi na kompyuta nchini.
Amebainisha kuwa, Serikali wataendelea kusaidia jinsia ya kike katika ukuaji wa Teknolojia ya Kidijitali nchini kwani kundi hilo lilikuwa limeachwa nyuma.
"Niwapongeze Unesco na Chuo kikuu cha BNU, kwa kuleta mradi huu nchini, utakaowezesha mafunzo kwa wasichana na Wanawake katika mafunzo yao ya Kidijitali.
Mradi huu ni mpango wa kidijitali kwa wasichana na wanawake ambapo Serikali wameuchukua na kuuweka katika mpango wa kimaendeleo na sera ya elimu hapa nchini hivyo tunaendelea kuwapongeza wadau kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jinsia ya kike" amesema.
Aidha, amesema kuwa, mradi huo utaenda katika mikoa yote na unaigharimu kiasi cha Dollars Laki tatu na nusu (USD 300,000.50), ambao utaenda kwenye Vyuo vyote vya elimu na maeneo ya elimu nchini,.
Ameongeza kuwa, utakuwa chachu kubwa kwani takwimu upande wa wasichana na wanawake ni asilimia 30 chini ya wavulana na wanaume.
"Kwa upande wa kisayansi wasichana na wnnawake waliachwa nyuma hivyo lengo la mradi huu ni kupandisha kutoka kiwango hicho na kupata uwiano sawa.
Kwa kutambua hilo, Serikali iliweka malengo katika mipango ya miaka 50, kwa kuingiza sera yake kwenye elimu kwa wanawake kidijitali" amesema Abdul Mnonya.
Akihitimisha wakati wa ufunguzi huo, amesema Serikali itaendeleza mradi huo hata utakapokwisha kwani ni wa muhimu.
Post Comment
No comments