THAMANI YA PSSSF YAENDELEA KUPAA
Dodoma - Mtaalam wa Masuala ya Hifadhi ya Jamii kutoka, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (PSSSF), Valentino Maganga amesema thamani ya mfuko huo imeongezeka kutoka shilingi trilioni 6 hadi 10.
Maganga amesema hayo leo mjini Dodoma, wakati wa Kongamano la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini kwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Wadau hao ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), PSSSF, Taasisi ya Kuzuia na Kupamban na Rushwa (PCCB), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), TASHICO, PAJI na THRDC.
Maganga amesema kutokana na thamani ya mfuko huo kuendelea kukuwa kwa kasi wamekuwa na uhakika wa kuendelea kuwahudumia watumishi wastaafu kila mwezi na kuongeza uwekezaji wenye tija.
"Thamani ya PSSSF imezidi kukuwa Kwa kasi kubwa ambapo tumetoka kwenye thamani ya shilingi trilioni 6 hadi 10 kwa sasa hivyo ukuaji kufikia asilimia 36 kutoka 22," amesema.
Manganga ambaye pia ni mwanasheria wa PSSSF amesema ukuaji wa mfuko huo umekuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mtaalam huyo amesema PSSSF kwa sasa inalipa shilingi bilioni 70 kila mwezi, hiyo ikiwa ni sawa na zaidi ya shilingi bilioni 800 kwa mwaka.
Manganga amesema kwa sasa PSSSF imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 9 kwenye miradi mbalimbali kama majengo na hisa kwenye benki ambazo zinachangia ajira na mikopo kwa wananchi, hali ambayo inaschochea ukuaji wa uchumi kwa kasi.
"Tumeweka zaidi ya shilingi trilioni 9 kwenye majengo, miradi ya uzalishaji na benki ambazo zinatoa mikopo kwa wananchi," amesema.
Aidha, amesema katika kuhakikisha PSSSF inafikia asilimia 40 ya viwango vya ukuaji kimataifa wanatarajia kuongeza nguvu kwenye eneo la fedha, rasilimali watu, matumizi ya TEHAMA na kuboresha ushirikiano na wadau kupitia kauli mbiu yao ya leo kesho pamoja.
meendelea mchang kufanikiwa kuongeza kiwango cha maendeleo kutoka asilimia 22 mwaka 2023 hadi asilimia 36 mwaka 2024/2025.
Lengo hili linakaribia kufikiwa kwa kiwango cha asilimia 40 kilichopendekezwa kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Hayo yamesemwa leo, Machi 14, 2025, na Mwanasheria Mkuu wa PSSSF, Valentino Maganga, alipokuwa akitoa taarifa kwenye Mkutano wa Wadau wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-Tan) 2025, uliofanyika Jijini Dodoma.
Maganga amesema mfuko huo umefanikiwa kuongeza thamani ya uwekezaji kutoka trilioni 6 hadi trilioni 10, hatua inayochochea maendeleo ya uchumi wa nchi.
Vilevile, ameongeza kuwa dhamana za uwekezaji zilizopo kwenye taasisi za kifedha, kama vile benki na majumba, zenye thamani ya Shilingi Trilioni 9, zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na ukuaji wa uchumi.
Aidha, amesema PSSSF inalipa pensheni kwa wastafu kila mwezi kiasi cha Shilingi Bilioni 70, na kwa mwaka ni zaidi ya Shilingi Bilioni 800, fedha ambazo huchochea shughuli za uchumi na kusaidia katika uwekezaji unaoingizia mapato Serikali.
Awali akiwakaribisha wageni Mwenyekiti wa MISA-TAN Edwin Soko amesema wameamua kuja na kongamano hilo ili kutoa fursa kwa wadau kama PSSSF na wengine wanapata fursa ya kuzungumza na kufafanua mambo wanayoyasimamia.
Soko amesema wao kama wanahabari wanaamini wakishirikiana katika kujadili mambo ya nchi mabadiliko yanaweza kutokea kwa haraka.
Post Comment
No comments