ORODHA YA MAJINA YALIYOPITISHWA NA KAMATI KUU CCM KUGOMBEA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea
ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye
mkutano wa Bunge ujao.
Akisoma
majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni
mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.
Mchanganuo
Miongoni
mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6
watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa
kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na
wawili watatokea Tanzania Visiwani.
Walioteuliwa
kugombea nafasi hizo ni;
Wanawake
Tanzania Bara;
Zainabu Rashid Mafaume Kawawa
Happiness Elias Lugiko
Fancy Haji Nkuhi
Happiness Ngoti Mgalula
Wanaume
Tanzania Bara;
Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe
Adam Omari Kimbisa
Anamringi Issay Macha
Charles Makongoro Nyerere
Wanawake
Zanzibar;
Maryam Ussi Yahya
Rabia Abdallah Hamid
Wanaume
Zanzibar;
Abdallah Hasnu Makame
Mohammed Yussuf Nuh
Miongoni
wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita
watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM.
No comments