RONALDO ATWAA TUZO YA BALLON D’OR. MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2016,
Mshabuliaji
wa Real Madrid amefunga mwaka kwa style ya pekee huku umri ukionekana kuelekea
ukingo kwani mwaka huu amefunga magoli mawili ya Uefa Champions ila ndo mshindi
wa Ballon d’Or.
Maana
amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or .
Ronaldo sasa anaichukua mara ya nne, akiwa alianza mwaka 2008 akiwa Manchester
United na alipoingia Madrid, unaweza kusema hii ni ‘hat trick’.
Kabla
haijawa Ballon d’Or, Ronaldo alichukua mwaka 2008, Messi akachukua mwaka 2009.
Baada
ya kuwa Ballon d’Or, Messi amechukua mara nne miaka ya 2011, 2012, 2013 na
2015. Huku Ronaldo akiwa amechukua mara tatu katika miaka ya 2013, 2014 na
2016.
Kumbuka
alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, akashinda Kombe la Euro
akiwa na Ureno.
Leo
amebeba kura zaidi kati ya 173 zilizopigwa na waandishi duniani kote kwa
usimamiza wa jarida maarufu la Ufaransa la France Football na kuwapiga bao
Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Luis Suarez na Lionel Messi, wote wa
Barcelona.
No comments