MAFIA BOXING PROMOTION YAGAWA MITUNGI YA GESI KUELEKEA PAMBANO LA AMIR MATUMLA NA PAUL AMAVILA
Dar es salaam - Wapenzi wa mchezo wa masungwi leo February 28 watashuhudia Mapambano makali 14 yatakayofanyika katika Viwanja vya Magomeni Sokoni ambapo Men Card wa Mchezo huo Amiri Matumla kutoka Tanzania na Paul Amavila kutoka Namibia.
Akizungumza kuelekea pambano hilo lilopewa maarufu kama "Knock Out ya Mama" ambalo limeingia msimu wa tatu amesema kuwa katika msimu huu limekuja kivyengine kwa kugawa majiko ya gesi kwa wamama Ntilie wa magomeni sokoni na zoezi hilo litakua endelevu.
Akizungumzua maandalizi kuelekea Pambano hilo ltakalo wahusisha mabondia kutoka ndani na nje ya nchi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila
"Jana kulikuwa na zoezi la kupima uzito na face-off kwa mabondia wanaotarajiwa kushuka ulingoni katika mapambano ya raundi sita na nane, yakiwemo yale ya main event". Alisema Zayumba.
Awali akizungumza zoezi la ugawaji wa gesi amesema lengo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia kama gesi na umeme badala ya kuni na mkaa.
Kwa upende wao baadhi ya mama lishe waliopokea mitungi washukuru Mafia Boxing Promotion kwa kutambua umuhimu wa kusaidia jamii na kuunga mkono sera ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhusu nishati safi ya kupikia.
Katika zoezi la kupima uzito, Rashid Matumla, bondia mstaafu na baba wa Amiri Matumla, ambaye anapigana kwenye main card, alisema kuwa mwanawe amejiandaa vizuri na ana nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya ulingo.
Kwa upande wake bondia Amiri Matumla ameahidi kutoa ushindi mnono dhidi ya mpinzani wake, Paulo Amavila kutoka Namibia, huku Amavila akijigamba kuwa Matumla bado ni mdogo kwake na hana nafasi ya kushinda.
Naye Promota mkongwe, J. Msangi, aliwapongeza uongozi wa Mafia Boxing Promotion kwa jitihada zao katika kuendeleza mchezo wa ngumi, akisema kuwa wao walifungua njia na sasa Mafia Boxing wanaendeleza kwa kiwango cha juu, huku akitabiri Tanzania kupaa zaidi kimataifa katika masumbwi.
Msimu wa tatu wa Knock out ya mama umekua wa kipekee zaidi ambapo mabondia wenye uwezo watapanda ulingoni kutoa burudani ya kutosha.
No comments