VETA WABAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA MIAkA 50 YA UTOAJI MAFUNZO


Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Dar es Salaam ikiwa katika maazimisho ya miaka 50 ya utoaji mafunzo na miaka 30 ya VETA Kanda hiyo ina jivunia mafanikio makubwa ya utoaji mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali.

Akizungumzia mafanikio ya VETA Kanda ya Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Wilhard Edward Soko, Mratibu wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Florence Kapinga amesema tunajivunia mafanikio makubwa walioyapata VETA katika kipindi chote cha miaka 30 tangu kuanzishwa mwaka 1968 pia ameelezea mafanikio kadhaa waliyoyapata kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa wameptana vifaa vipya ya TEHAMA, Vifaa vya Printing, Vifaa vya masomo ya electronics na vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya Chang'ombe na Kipawa.
Amesema kumekia naongezoka la udahili, ongezeko la vyuo kutoka vyuo viwili hadi kufikia vyuo vitano ambapo Vyuo vitatu vinavyojengwa katika Wilaya ya Ubungo, Kinondoni na Kigamboni ujenzi unaendelea na unatarajiwa kukamilika 2026.

Alisema Majukumu makubwa ya VETA Kanda ya Dar es Salaam ni kutoa mafunzo, kusimamia mafunzo, kuratibu mafunzo, kuhamasisha na kutahini wahitimu wa mafunzo kwa ngazi ya mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi na kwa mwaka wamefanikiwa kutahini wanafunzi wapatao 6,000/= kwa Kanda hiyo ambapo kumekia na ongezeko kubwa la wanafunzi wa kike kwa asilimia 30 kwa kujiunga na fani za filter na umeme ambazo zamani zilikua zikionekana kuwa za wanaume.

Aidha, Mratibu Kapinga ameeleza kuwa VETA Kanda ya Dar es Salaam wamekuana mashirikiano na wadau mbalimbali kama vile Benki ya KCB, VCO TZ, Airtel, SKM Signal, pia kufanya vipindi katika vyombo vya habari vikitangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kanda ikiwemo kutangaza nafasi za masomo na kushiriki maonesho
Ameeleza changomoto wanazokabiliana nazo kwba ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi, fani mtambuka, kiingereza, mathematics, pamoja na vifaa vya kufundishia, uhaba wa majengo na nafasi finyu ya madarasa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.

Akizungumza katika Maonesho ya Vitendo yaliyoandaliwa katika Kanda ya Dar es Salaam Mwalimu wa Eletronic, bwana Ricky Sambo amesema Kanda ya Dar es Salaam ina vituo vitatu vyakutolea mafunzo ambavyo ni Kanda ya Dar es Salaam, Dar es Salaam, Kipawa -Tehama.

Mafunzo yanayotolewa katika Vyuo hivyo ni ya muda mfupi na ya muda mrefu katika fani za Umeme, Maabara, Ushonaji, Uchapaji, Uchoraji wa ramani na usanifu wa majengo, Electronics, ICT, Mechatronics, Dsct, ufundi seremala, fani ya mabomba, Uchomeleaji pamoja na ubunifu mbalimbali.
Mwalimu Sambo amesema ada ya chuo kwa fani zote kwa mafunzo yote ada yake haizidi shilingi 120,000 kwa bweni na 60,000/=kwa wanafunzi wa kutwa na gharama nyingine zinawezeshwa na Serikali.

Naye Kaimu Msajili VETA Chang'ombe ,Ziada Shekimweri amesema wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi ni wengi na pia ameipongeza serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu mbalimbali yakiwemo madarasa na ujenzi wa vyuo vya VETA kwa Kila Wilaya.
Kwa upande wa wanafunzi akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzie Rafaeli Njilaren Mmanyi ambaye Yuko mwaka wa pili katika fani ya The Toyota Hybrid System mfumo ambao unatumia vitu viwili yaani injini na mota kwa ajili ya magari ameiashukuru serikali kwa udhamini wanaotoa kuwadhamini wanafunzi katika fani mbalimbali   

Alisema kupitia Maonesho hayo ambayo yaliaanza Machi 11,2025 na yatahitimishwa Machi 14, 2025 katika Viwanja VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.

No comments