TIGO YATANGAZA KUWASILISHA DOKEZO LA MUHTASARI KUHUSU PENDEKEZO LA AWALI LA KUUZA HISA ZAKE KWA UMMA
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi
wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo balozi (mstaafu) Ami Mpungwe (katikati)
akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez
wakikabidhi kabrasha lenye mapendekezo ya kuomba kuorodhesha hisa katika soko
la hisa la Dar Es Salaam (DSE) kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa soko hilo, Moremi
Marwa.
Dar es
Salaam – Desemba 8, 2016 –Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya MIC Tanzania
Limited (Tigo) imetangaza rasmi kuwasilisha muhtasari na maombi ya awali katika
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa Dar es Salaam
(DSE) kuhusiana na mapendekezo ya awali ya kuorodhesha hisa zake katika Soko la
Hisa la Dar es Salaam.
Uuzwaji
wa hisa hizo unatarajiwa kuanza mara baada ya CMSA na DSE kumaliza mchakato wa
mapitio kulingana na masharti yanayohusu soko la hisa.
Akizungumza
wakati wa uwasilishaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez,
alisema: “Tunayo furaha kutangazia umma kuhusu uwasilishaji wa muhtasari wetu
ili mchakato uanze rasmi na kwamba tutawapatia wateja wetu, wafanyakazi wetu na
Watanzania kwa ujumla fursa ya kuwa wamiliki wa hisa ndani ya kampuni yetu.”
Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi ya MIC Tanzania Limited, Balozi (Mstaafu) Ami Mpungwe
aliongeza kuwa: “uwasilishaji huu ni hatua muhimu katika historia ya kampuni na
kwamba utawapatia Watanzania wote fursa sawa ya kushiriki katika mtaji wa
kampuni yetu katika siku za usoni. Tutafanya kazi pamoja na mamlaka za
usimamizi kuhakikisha mchakato huu unafanyika ipasavyo.”
No comments