Breaking News

MAFUFU, SHAMSA FORD NA STAMINA WAHAMIA CCM, KUFANYA ZIARA KUELEZA MAFANIKIO YA DKT. SAMIA "ASANTE MAMA"

Msanii wa filamu, Jimmy Mafufu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uamuzi wake wa kuhamia chama cha mapinduzi (CCM) mkutano uliofanyika katika hotel ya serena jijii Dar es salaam
Shamsa Ford aliyekuwa kada wa chadema akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uamuzi wake wa kuhamia chama cha mapinduzi (CCM) mkutano uliofanyika katika hotel ya serena jijii Dar es salaam.
Msanii wa maigizo Single mtambile maarufu kama Richie akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu uliofanyika katika hotel ya serena jijii Dar es salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Boniventure Kabongo maarufu kama ‘Stamina" akielezea sababu za kujiunga na CCM katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya serena jijii Dar es salaam.

Dar es salaam - Wasanii wa filamu, Jimmy Mafufu na Shamsa Ford wametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wakiwa chini ya Taasisi ya Mabalozi wa Mama na wataanza ziara nchi nzima kutangaza mafanikio ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassang yenye kaulimbiu ‘Asante Mama’.

Nyota hao ambao wameamua kujiunga CCM wakitokea katika vyama mbalimbali ikiwemo Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) wamekiri sababu kubwa ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na Dkt Samia ambayo inafanya taifa kukua kiuchumi.

Mafufu akizungumza amesema binafsi nimeamua kuijunga CCM baada ya kubaini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita imefanya makubwa kwa Watanzania wakiwemo wasanii ambao wamepewa mikopo ya kuinua kazi zao.

“Licha ya kwamba mimi na Shamsha tulikuwa upinzani, mikopo hiyo inayotolewa na Rais wetu kwa wasanii haikutubagua, pia Serikali yetu imefanya mambo makubwa ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo kama Barabara, Bwawa la Mwalimu Nyerere, Reli ya SGR, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato, hayo ni sehemu yaliyotukusukuma kujiunga CCM,”. Alisema Mafufu.
Alisema tangu Rais Dkt. Samia, aingie madarakani hajashindwa, ametekeleza miradi yote iliyoachwa na marehemu Rais Dkt John Magufuli, hali ambayo imefanya kutoona umuhimu wa kuwa wapinzani.

Kwa upande wake Shamsa Ford amese8 anajivunia kujiunga na CCM na nitoe wito kwa wasanii wengine ambao wako katika vyama vya upinzani kujiunga na ccm ili kuunganisha nguvu ya pamoja kutangaza miradi ya maendeleo ambayo imefanikisha kustawisha uchumi wa Tanzania.

Nae msanii wa maigizo Single mtambile maarufu kama Richie ambaye ni diwani wa CCM amesema kwa nafasi aliyonayo anaamini watatangaza, miradi yote ambayo imefanya vizuri kwa maslahi ya watanzania ili kila mmoja ajue.
.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni miradi ya Elimu, Afya, Usafiri wa Anga na Reli ya SGR, Bandari na mingineyo inayoifanya Tanzania kuwa mfamo wa kuigwa katika mataifa mengine.

Wasanii kutoka vyama vya upinzani ni Salum Mchoma (Chiki), Single Mtambalike ‘Richt Ritch’, Rashidi Mwishehe ‘Kingwendu’ Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’ na wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Boniventure Kabongo ‘Stamina, Juma Kassim ‘Nature ‘Sir Nature’, Amani Temba ‘Capt Temba, Richard Shauri ‘Ritch One’ na wengine na lengo lao ni kutangaza miradi yote ambayo imetekelezwa chini ya Rais Samia.

No comments