Breaking News

BAJAJI FC WAIBUKA MABINGWA KUMBILAMOTO CUP 2025

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema awamu ya pili ya Michuano ya Kumbilamoto Cup itawafikia wananchi wa kata nyingine za wilaya ya ilala ili kuendelea kutoa fursa za vijana wengi kuonesha vipaji vyao.

Mhe Meya ameyasema hayo jana februari 28, 2025 katika viwanja vya Msikate tamaa vilivyopo Vingunguti ambapo ulichezwa mchezo wa fainali ya michuano kati ya Bajaji Fc dhidi ya Saigon Fc huku timu ya Bajaji ikiibuka Mabingwa wa michuajo hiyo kwa kuifunga Saigon magoli 2 - 0.
"Tuna mpango wa kuboresha viwanja vya Michezo ndani ya Jiji letu tumeanza na uwanja wa shule ya Benjamin mkapa tayari mkandarasi amepatikana pia tutatanua wigo wa michuano hii kufika kata nyingine ili kuongeza fursa za vijana kuonesha vipaji vyao" amesema kumbilamoto

Aidha katika michuano hiyo ya Kumbilamoto Cup mshindi wa kwanza ambaye ndiye Bingwa Bajaji Fc amepata Kikombe na fedha kiasi cha Tsh Milioni moja na Ng'ombe mmoja , huku mshindi wa pili akipata Mbuzi wawili, Jezi na mipira.

Michuano hiyo imetamatika rasmi leo February 28, 2025







No comments