VIDEO: CRJE LAUNCHES PENINSULAR NOBLE CENTER BUILDING WORTH U$40 MIL IN TANZANIA'S BUSINESS CAPITAL

Kampuni ya CRJE Investment (EA) kutoka nchini China imezindua jengo jipya la kibiashara, Peninsular Noble Center ambalo limejengwa kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 40 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuchochea uchumi wa nchi.

Jengo hilo ambalo lipo Oysterbay, jijini Dar es Salaam lilianza kujengwa mwaka 2019 ni maalumu kwa maduka makubwa (supermarkets) na lina nafasi za ofisi, maeneo ya mazoezi na migahawa.

"Tumezindua jengo letu la Peninsula Noble Centre hapa Oysterbay, Dar es Salaam ambapo tumeshaingia katika mikataba na baadhi ya Mabenki, supermarkets na migahawa ambapo watafungua ofisi zao hapa katika jengo hili la kibiashara,” Meneja Mkuu wa Kampuni ya CRJE Investment (EA) Bwana Li Tianye alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa CRJE Investment (EA) Liu Dan alisema kuwa jengo la Peninsula Noble Center lenye mazingira bora ya kibiashara lilianza kujengwa mwaka wa 2019 lakini walishindwa kuendelea kutokana na mlipuko wa COVID-19. lakini waliendelea na ujenzi tena mwaka 2023 na kufanikiwa kumaliza ujenzi na hivyo kuzinduliwa kwa 1 Aprili 2025.

“Tunawakalibisha wateja wetu wote waweze kuja kufungua ofisi na maduka kwasababu tunajivunia mazingira bora ya biashara katika jengo hili," alisema Bi Liu Dan  

No comments