Breaking News

SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA UVUVI WA KIDIGITALI

Na Neema Mpaka, Dar es salaam - Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Sapphire Imezindua mfumo wa uvuvi wa kisasa utakaohusisha njia za kidigitali zitakazowasaidia wavuvi kujua maeneo ya samaki pamoja na hali ya hewa kwa siku husika.

Akizungumza na wavuvi katika soko la samaki- Feri- Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amewaasa wavuvi kujiunga katika mfumo huo utakaowawezesha kujiinua kiuchumi kupitia uvuvi wa kisasa.

"Mfumo huu wa uvuvi wa kidigitali unaojulikana kama Vua na Uza Kidigitali ni njia bora utakaowawezesha wavuvi kuvua kisasa na umeunganishwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), ili mvuvi aweze kujua hali ya hewa utakavyokuuwa majini kabla ya kwenda kuvua," amesema DKT. EDWIN MHEDE  

 Aidha amesema wavuvi wamepata uhakika wa kuvua kufuatia Kujua hali ya hewa na mahali samaki wanapopatikana kwa wingi.

Alikadhalika ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es, Elihuruma Mabelya kuhusu kuwatengenezea mazingira rafiki ya kupata mikopo.

"Tengenezeni mazingira rafiki ya kuwapatia mikopo Hawa wavuvi kwa kuwa tayari wapo kwenye mifumo rasmi," amesema DKT. MHEDE
 
Aidha daktari Mhede ametoa wito kwa wavuvi kujisajili kwa wingi kwani mfumo huo ni Bure kujisajili ili kuongeza ukubwa wa soko.
Awali mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema sekta ya uvuvi imeendelea kuchangia ukuaji wa mapato katika jiji la ilala hivyo uzinduzi wa mfumo huo utaongeza ufanisi katika sekta ya uvuvi

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa soko la uvuvi la samaki feri Ndugu Nassoro Mbaga amesema wanaishukuru serikali kwa Kuja na mfumo huu wa Vua Uza na Nunua Samaki Kigiditali watatumia vyema mfumo huo ili kujiinua kiuchumi.


No comments