KAMATI YA BUNGE YAIPA HEKO NCAA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU KARATU
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro tarehe 23-24 Machi, 2025 na kuipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa uboreshaji wa miundombinu ya Utalii na ujenzi wa jengo la Makao makuu ya NCAA nje ya Hifadhi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma, Augustine Vuma (Mb) amesema kuwa, kamati wanaipongeza NCAA kwa ujenzi wa Jengo la Makao makuu ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha shughuli za uhifadhi na kupunguza shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya Ngorongoro.
“Kamati ya PIC imekagua jengo hili na miundombinu mingine ya utalii, tunawapongeza kwa ujenzi wa jengo hili lenye kiwango kinachoendana na thamani ya fedha, hakikisheni mnamsimamia mkandarasi kumaliza ujenzi huu kwa wakati ili jengo hili lizinduliwe naa kutumika kwa kazi za Mamlaka na kutimiza kusudio la Serikali la kuboresha uhifadhi na kupunguza shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi” alisisitiza Vuma.
Wabunge wa Kamati hiyo wameipongeza NCAA kwa uboresjaji wa miundombinu ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii hali iliyopelekea ongezeko la Mapato ambayo yanapoingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali yanasaidia kuwekeza katika miradi mingine na kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) ameielezea kamati hiyo kuwa Bodi na menejimenti ya NCAA itaendelea kuhakikisha kuwa miundombinu inayojengwa ikiwemo jengo la Makao makuu na miradi mingine inasimamiwa kikamilifu na kufanyiwa maboresho ya mara kwa mara ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wageni wanaotembelea NCAA.
Akitoa taarifa ya Mradi, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Humphrey Swai ameeleza kuwa ujenzi wa jengo la Makao makuu ya NCAA unaotekelezwa na kampuni ya China Jiangxi for International Economic and Technical cooperation Co. Ltd umegharimu shilingi Bilioni 10,474,526,694.25.
Ambapo fedha hiyo imehusiaha ujenzi wa jengo la Makao Makuu, Nyumba ya kamaishna wa Uhifadhi na Nyumba mbili za manaibu Kamishna wa Uhifadhi ambapo ujenzi umeshafikia asilimia 85 na ujenzi unatarajiwa kukamilika, Mei 30, 2025.
Post Comment
No comments