BARAZA LA WAFANYAKAZI BRELA LAZINDULIWA MKOANI MOROGORO
Godfrey Nyaisa, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) akizungumza na wajumbe wa Baraza kwenye ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi na kikao cha kwanza cha Baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 mkoani Morogoro.
Christina Matage Ofisa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu akitoa mafunzo juu ya namna ya uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi kwa wajumbe wapya wa baraza la wafanyakazi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mkoani Morogoro
Morogoro - Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo Februari 6, 2025 mkoani Morogoro, imezindua Baraza la Wafanyakazi pamoja na kufanya kikao cha Kwanza kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Akizungumza Katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la hilo, Godfrey Nyaisa amewakumbusha Wajumbe kutekeleza majukumu yao ili kuleta tija na ufanisi mahali pa kazi.
“Baraza hili la Wafanyakazi wa BRELA lina jukumu la kipekee la kuchangia katika kuweka mazingira bora ya kazi yenye kuongeza tija, ushirikiano na maendeleo ya wafanyakazi, ambayo ndio uti wa mgongo wa mafanikio ya Taasisi". Alisema Nyaisa na kiongeza kuwa
"Tunapokutana hapa ni fursa ya kutafakari mafanikio, kujadili changamoto na kuweka mikakati ya pamoja kwa mustakabali wa Taasisi yetu.”
Alisema Baraza la Wafanyakazi litakuwa na jukumu la kuishauri wakala kuhusu masuala yanayohusu maslahi ya watumishi, utekelezaji wa mipango na makisio ya mapato na matumizi ya Wakala, kupokea taarifa ya utekelezaji wa wakala na kutoa ushauri, kudumisha ushirikiano kati ya watumishi na wakala katika uendeshaji wa Wakala na kushauri kuhusu ustawi wa wakala na maendeleo ya watumishi.
Ameongeza kuwa sambamba na uzinduzi wa baraza hilo ambalo litakuwa likifanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Taasisi kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kuangalia malengo yaliyopangwa,
utekelezaji wa majukumu, changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji pamoja na mikakati ya kukabiliana na changamoto husika.
Aidha bw. Nyaisa alibainisha kuwa baraza litajadili na kupitisha makadirio ya Bajeti ya
Wakala kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika kikao hicho baraza pia lilifanya uchaguzi ambapo Peter Riwa, Ofisa Leseni Mwandamizi alichaguliwa kuwa Katibu na Gift Wazingwa, Ofisa Usajili alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi.
Mkutano huo wa ufunguzi na uchaguzi ulishuhudiwa na Brendan Maro, Dkt. Hussein Mugyabuso kutoka Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) na Christina Matage kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Post Comment
No comments