RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI UFUNGUZI MKUTANO WA 11 WA MERCK FOUNDATION
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima (kulia kwake) CEO of Merck Foundation Senator Dr. Rasha Kelej na (kushoto kwake) Chairman of Merck Foundation Board of Trustees & Former Chairman of Executive Board of E. Merck KG, Prof. Dr. Frank Stangenberg - Haverkamp katika mkutano uliofanyika katika hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (kulia kwake) CEO of Merck Foundation Senator Dr. Rasha Kelej mkutano uliofanyika katika hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam
.Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa 11 wa kimataifa wa Merck Foundation utakaoganyika Oktoba 29 na 30 jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika Kikao na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima amesema
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni kutambua jitihada zake za uwekezaji katika sekta ya afya hasa katika afya ya mama na mtoto.
"Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa 11 wa kimataifa kutokana na jitihada Dkt. Samia katika uwekezaji katika sekta ya afya hasa afya ya mama na mtoto ambazo inafanya vizuri, pamoja na uwepo wa mazingira mazuri ya amani na utulivu kutokana na uongozi bora na wa kupigiwa mfano wa Rais Samia". Alisema Dkt. Gwajima.
Alisema mkutano huo ambao washiriki zaidi ya washiriki 600 kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria na wengine kufatilia moja kwa njia ya mtandao
Amezitaja baadhi ya nchi zitakazoshiriki mkutano huo kuwa ni Zambia, Nigeria, Zimbabwe, Ghana, Botswana, Kenya, Malawi, Afrika ya kati, Guinea Bissau, Afrika ya kusini na wenyeji Tanzania.
No comments