Breaking News

DKT JINGU AONGOZA KIKAO CHA MAPITIO NA UTEKELEZAJI WA HUDUMA ZA CHANJO NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu  leo Septemba 18, 2024 ameongoza  kikao cha kitaifa cha uratibu wa huduma za chanjo nchini lengo ikiwa kufanya mapitio ya taarifa za utekelezaji wa huduma za chanjo nchini.

Kikao hicho ambacho kimefanyika ofisi ndogo za wizara ya Afya NIMR Jijini Dar es salaam, chini ya kamati wamepitia taarifa utekelezaji wa Afua za Afya na kuridhishwa na utekelezaji wa afua hizo nchini kwa kipindi cha Januari hadi Julai 2024.

Kamati ya taifa ya huduma za chanjo imeadhimia kushirikiana na kuongeza nguvu ili kuchochea tija, ufanisi na ubunifu kwenye utekelezaji wa huduma za chanjo nchini.

Katibu Mkuu Dkt. Jingu aliambatana pia  na Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania (WHO) Dkt. Charles Sagoe-Moses, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara Dkt. Ntuli Kapologwe na Mkurugenzi wa mpango IVD Dkt Georgina Joachim


No comments