Breaking News

IVAN MAGANZA RASMI MWENYEKITI MPYA WA CHAMA CHA TLP TAIFA

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Injinia Ivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo, bwana Rashid Amir, amesema Bw. Maganza ameshinda kwa kupata kura 33 kati ya kura zote za wajumbe wa mkutano huo 45 ambapo mshindani wake mkuu katika uchaguzi huo huku Bwana Kchanzoro Mwanga akipata kura kumi (10) na kushika nafasi ya pili huku Bwana Stanley Ndomigoba akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura tatu (3) huku Abuu Changawa na Richard Lyimo wakipata (0)

Akizungumza mara baada kutangazwa kuwa mshindi bwana Maganza ameahidi kushirikia na wanachama wote wenye nia ya shati na wapenda mabadiliko kwa lengo la kukijenga upya chama hicho kuwa moja ya chama makini cha siasa na akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange.

“Kwanza napenda kuwashikuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuniamini na kunichagua ila nitoe rai kwa Wale wote ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia hili nibaki na watu makini na wenye kiu ya kuona chama kinakuwa na wanaoweza kufanya kazi,” Alisema Bw. Maganza.

Bw. Maganza pia ametumia mda huo kutangaza safu ya uongozi ambayo atafanya nayo kazi kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na kuwa moja chama tishio nchini kwa kumteua Bi. Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu Taifa kufatia alieluwa katibu mkuu wa chama hicho bwana Richard Lyimo kutimka na kuongeza kuwa ndani ya miezi mitatu kuunda upya sekretarieti ya chama hicho.
Mapema Makamu Mwenyekiti TLP Taifa, Bi.Dominata Rwechungura akizungumzia hatua na chamamoto mbalimbali za mchakato mzima wa uchaguzi mkuu huo alisema chama kimepitia wakati mgumu sana kufatia kuvurugika.

"Zoezi la kuandaa uchaguzi limekuwa likipitia changamoto nyingi kila mra kutukiihisha uchaguzi na kupelekea kushindwa kufanyika jambo lilopelekea kuandika barua mara kwa mara kwa Msajili wa vyama vya siasa ambaye ni mlenzi wa vyama leo tunahitimisha rasmi uchaguzi nitoe rai kwa wajumbe na wanachama kushikamana kujenga chama ambacho hayati Mrema amekipigania kwa jasho na damu". Alisema Rwechungura .

kwa upande wake katibu Mwenezi wa chama hicho Bwana Geofray Stephen Laizar amesema ni wakati wa wanachama wa chama hicho kushikamana na kuwa pamoja pasipo kuangali dini wala kabila na kuondoa makundi katika chama hili kukijenga upya chama.

Amesema mara baada ya kumpata mwenyekiti mpya chama kitaunda safu mpya ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kisha kumsimamisha mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwakani 2025.

No comments