CHAMA CHA NATIONAL LEAGUE FOR DEMOCRACY (NLD) CHAVUNA WANACHAMA
Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo akimpatia KADI ya uanachama aliyekuwa mgombea Ubunge Kibaha Mjini 2020 na Mgombea Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kupitia Chama cha ADC, Bi. Schola Kahana makao makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo akimpatia kadi ya uanachama aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo Kanda ya Pwani Mariam Sijaona makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam
Wanachama zaidi ya 150 kutoka ADC na ACT wamejiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo. Wanachama hao, wakiongozwa na Mariam Sijaona aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ACT Wazalendo na Scola Kahana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti bara kupitia ADC na mgombea ubunge jimbo la kibaha katika uchaguzi wa 2020, leo tarehe 29-09-2024 wamejiunga na Chama cha NLD.
Mhe. Doyo, pamoja na viongozi wengine wa NLD, akiwemo Makamo Mwenyekiti Bara, Mhe. Khamis Said Hamad, waliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa na wanachama wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya NLD. Wanachama hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na Chama cha NLD kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kuunga mkono juhudi za Mhe. Doyo katika kukuza demokrasia nchini.
"Tunajua chama chetu kipya hakina ruzuku, lakini tupo tayari kukaa na njaa ili kupigania demokrasia ya kweli na hatimaye chama chetu kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo," walisisitiza wana chama hao.
Mhe. Doyo aliwasihi wanachama hao wapya kusoma Itikadi ya NLD, akisisitiza kuwa Itikadi ya chama hicho imebeba uzalendo, haki, na maendeleo.
Katika hatua nyingine Mhe. Doyo alibainisha kuwa chama kinatarajia kufanya ziara ya kujitambulisha kwa wanachama pamoja na kutangaza sera za chama hicho nchini nzima ziara itakayoanza kuanzia Oktoba 30 ikianzia mkoani Tanga, Pemba, kanda ya ziwa na mikoa ya kanda ya kaskazini.
No comments