Breaking News

ZAIDI YA WASHIRIKI 600 KUJITOKEZA MAONESHO YA MADINI MKOANI GEITA

Zaidi ya Washiriki 600 wamejitokeza kushiriki Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yaliyoanza leo Oktoba 03, 2024 katika viwanja vya Bomba Mbili Mkoani Geita ambapo Wizara ya Madini na Taasisi zake wanashiki katika kutoa elimu kuhusu shughuli za Sekta ya Madini.

Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Oktoba 5, 2024 ambapo Mgeni rasmi katika ufunguzi huo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko na yanategemewa kuhitimishwa Oktoba 13, 2024 na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella ametoa wito kwa wananchi kutembelea Maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Bomba Mbili kwa lengo la kujifunza uchimbaji salama na mnyororo mzima wa uongezaji thamani Madini.
Aidha, Shigella amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita imelenga kuyaboesha Maonesho kutoka kwenye Maonesho ya Kitaifa na kuyafanya kuwa Maonesho ya Kimataifa yatakayokuwa yanafanyika Kila Mwaka Mkoani humo.

Maonesho hayo, yamebebwa na Kauli mbiu isemayo, "Matumizi ya Teknolojia Sahihi na Nishati Safi katika Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Endelevu"



No comments