Breaking News

ITUTU MWENYEKITI MPYA CHAMA CHA ADC, AAHIDI KUSHIRIKIANA NA DOYO

Dar es Salaam.
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), kimepata viongozi wapya wa kitaifa, huku aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Shabani Itutu akiibuka na ushindi kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa.

Itutu amemshinda Doyo Hassan aliyekuwa Katibu Mkuu wa nne chama kwa kupata kura 121 dhidi ya Doyo aliyepata 70, kati ya kufa 192 zilizopigwa huku kura moja ikiharibika katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi Juni 29, 2024 katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam

Viongozi walioshinda katika uchaguzi huo ni wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Bi. Azizi amesema mgombea wa nafasi hiyo, Bi. Fatuma Salehe amepata kura 120 dhidi ya mpinzani wake Shara Amran aliyepata kura 49, ambapo kura nne zikiharibika.

kwa upende wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti - Bara, bwana Hassan Mvungi amepata kura 135 dhidi ya Scola Kahana aliyepata kura 35.ambapo Kura tatu zimeharibika.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, bwana Itutu ameahidi kutoa ushirikiano kwa mgombea aliyekuwa akishindana naye, akiwashukuru wapigakura kwa ushirikiano waliouonyesha.

Amesema Doyo ni mmoha ya wanachama wa siku nyingi waliyeanza naye ndani ya chama hicho, hivyo wataenda pamoja na kufanya naye kazi bila kujali chochote.

"Chama hiki sasa ni kikubwa kama mnavyoona mkutano huu ni wa kipekee, hata msajili amekiona," Alisema Bw. Itutu.

Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, bwana Mohamed Ali Ahmed amekipongeza chama hicho kwa kuweka utaratibu wa ukomo wa uongozi.
Amesema chama hicho ni kichanga lakini kimezidi kukua kikiwa na wanasiasa wakongwe na wabobezi.

"Niwapongeze ADC ni kimojawapo kati ya vyama vichanga lakini kimeweka utaratibu mzuri wa kupokezana vijiti," Alisema Bw. Ahmed.

Amebainisha kuwa vipo baadhi ya vyama vya siasa (bila kuvitaja) ukiviangalia, unaona viongozi wake hawataki kutoka na wengine wakijaribu kuingia.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid awali aliwataka watakaochanguliwa kutokubali kuuza utu wao, kwa kuwa watakibomoa chama endapo wataingia kwenye rushwa.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa ADC, bwana Said Miraj Abdallah amesema sifa ya kiongozi mzuri ni yule anayefikiri kwa ajili ya anaowaongoza kwa kutumia akili.

No comments