Breaking News

DOYO: UCHAGUZI ULIKUWA NA UKIUKWAJI WA SHERIA NA KUTOZINGATIA KATIBA YA CHAMA

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), bwana Doyo Hassan Doyo amesema tayali amewasilisha barua ya wajumbe 70 kikata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi kilutokana na kutozingatia Katiba na kanuni za Chama.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Doyo ambaye pia ni katibu mkuu wa chama hicho amesema uchaguzi huo ni batili kutokana na kuwa na mapungufu mengi hivyo hawautambui na kushauri kuwa urudiwe tena na usimamiwe na Msajili wa vyama vya siasa.

"Tayari nimeshawasilisha rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo kutokana kukiuka kuvunjwa vifungu vya Katiba ya chama ikiwemo mkutano kuongozwa na Mwenyekiti anaemaliza muda wake badala ya Mwenyekiti wa muda anaeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Katiba ya chama". Alisema bw. Doyo na kuongeza kuwa

Alisema kwa mujibu wa kanuni mwenyekiti wa muda ndio anatakiwa kusimamia uchaguzi huo hivyo kitendo Cha Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid kusimamia mkutano Mkuu wote wa uchaguzi mpaka nafasi za makamu Mwenyekiti Kwa upande wa Bara na Zanzibar amevunja kanuni za Chama hivyo kuufanya uchaguzi huo kuwa ni batili.

Aliongeza taratibu kuwa katika uchaguzi huo uliofanyika June 29, 2024 jijini Dar es salaam zoezi zima la upigaji kura pia alikuzingatiwa kutokana na kuwa na wajumbe zaidi ya idadi ambayo iliyowasilishwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutokutumika ambayo ilionyesha kuwa jumla ya wajumbe halali wakutano huo ni 192 na hila wajumbe waliokuwepo siku ya uchaguzi na kupiga kura 200.

Alisema Viongozi waliochaguliwa wapya wengi ni ndugu Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid ambao amechagua mwenyewe hivyo inadhihirisha kuwa kua ajaenda na anakitaka Chama Kwa mgongo wa nyuma.

Aidha katika hatua nyingine Doyo amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumwamini na kumpigia Kura 70 kati ya wajumbe halali 192.

"Ndugu waandishi wa habari wote mashahidi pamoja na figizu zote zilizofanywa lakini tulikuwa watulivu kipindi chote cha uchaguzi na kufata utaratibu kwa kuwasilisha barua ya kukata rufaa kutokana na kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchauzi ulivyo endendeshwa na kama awatapata ushirikiano watachukua hatua zaidi kwa kwenda kuupinga mahakamani". Alisema Bw. Doyo. 

No comments